Jinsi ya kupiga simu za video katika WhatsApp.

Hatimaye mtandao wa WhatsApp umeanza kutoa huduma za simu za video kwa wateja wake, katika tangazo ambalo mtandao huo umelitoa WhatsApp inasema inataka huduma hii mpya iweze kuwafikia watumiaji wote wa simu tofauti na mitandao mingine ambayo inatoa huduma hiyo.
Screenshot kuonesha huduma hiyo mpya katika Whatsapp
Je ni lini huduma hii itawafikia watumiaji hasa sisi wa Tanzania!?
Ingawa tangazo limetolewa leo ila tumekuwa tukisema hapa kwamba huduma hizi husambazwa kwa watumiaji kwa awamu mbalimbali na pengine itachukua zaidi ya wiki kuwafikia watumiaji wote zaidi ya bilioni moja wa mtandao huu. Kwa kuanzia wateja walio katika masoko makubwa kama Marekani na Uingereza wataanza kupata huduma hii ya kupiga simu za video.
Muonekano wa huduma hiyo
Huduma hii inafanyaje kazi!?
Kwa kila mtumiaji wa App hii ya WhatsApp atahitaji kupakua na kusanikisha toleo jipya la app kisha baada ya hapo ili kupiga simu ya video utafuata utaratibu ule ule wa kupiga simu ya kawaida ila utakapo taka kupiga simu itakuuliza kama unataka kupiga simu ya kawaida ama ya video.
Bila shaka muonekano wa video katika simu ya video ni tofauti kwa kila aina ya simu na Os husika lakini kiujumla huduma hii itapatikana kwa aina zote za simu na aina zote za OS, pengine hii ni moja ya faida za WhatsApp ukilinganisha na huduma kama Facetime ambayo ipo katika iOS tuu.
Tungependa kusikia maoni yako kuhusu huduma za simu za video je!? unazitumia na kama jibu lako ni ndiyo unatumia huduma zipi zaidi?

Previous
Next Post »

Ads Inside Post