Full moon

Baada ya miaka 68 dunia itaweza kuuona mwezi ukiwa mkubwa na angavu zaidi katika tukio linalojulikana kwa kingereza Super-moon, tukio hili linategemewa kutokea siku ya kesho. Kwa mujibu wa mtandao wa
HAARETZ kwa mara ya mwisho tukio hili lilitokea Januari 1948 na baada ya kesho tukio hili linategemewa kutokea tena tarehe 25 mwezi Novemba mwaka 2034.
Mwezi  huizunguka dunia ambayo inalizunguka jua, katika mzunguko huu wa mwezi dunia na jua kila usiku mmoja jua huangaza miale yake katika kipande fulani cha uso wa mwezi. Katika mzunguko mmoja kuna wakati fulani mwezi huwa unatazamana na jua(yaani mwezi unakuwa katika mstari mmoja na jua huku dunia ikiwa kati yao) hapa uso mzima wa mwezi huangazwa na kuufanya uso mzima uonekane tukio hili linajulikana kama Fullmoon kwa kingereza.
Mchoro kuelezea tukio hilo
Full moon ni kitendo ambacho hutokea katika kila mzunguko wa mwezi kuizunguka dunia lakini kutokana na namna mzunguko huu ulivyo kuna nyakati mwezi unakuwa karibu na dunia zaidi, kipindi ambacho full moon inatokea wakati dunia ipo karibu zaidi na mwezi ndio huleta tukio ambalo tunaliita Super-moon.
Hili ni tukio kubwa katika sayansi ya anga hivyo ni jambo zuri kuwaelezea watoto pamoja na wengine ambao wanapenda sayansi.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post