Whatsapp yaboreshwa; Sasa unaweza kuchora kitu chochote kwenye picha/video

Siku zote katika biashara lazima uwe mjanja ili kuweza kuendelea kuwavutia wateja wako au hata kupata wateja wapya kutokana na ubora wa bidhaa zako; WhatsApp wameliona hilo na wao wameamua kuiboresha app yao.
Ulikuwa ukitamani kuona unaweza kuchora kitu chochote kwenye picha/video kabla ya kumtumia mtu/watu au hata kuiweka kama picha ya kuweza watu kukufahamu wewe ‘Display picture’ almaarufu kama dp ? Basi sasa unaweza kufanya hivyo kwenye whatsapp.
Kuweza kuchora kitu kwenye picha si jambo geni kwa watumiaji wa Snapchat na kwa hivi kari buni kwenye Instagram na iMessage.
Jinsi ya kuweza kupata maboresho mapya kwenye Whatsapp
Kwenye app yoyote ile ili kuweza kupata maboresho inapaswa programu tumishi iwe ni ya toleo jipya (latest version). Baada ya hapo utakapojaribu kuchagua au video basi kabla ya kuituma utaweza kuandika (caption)/kuchora kitu chochote katika picha au video hiyo.
Unaweza ukabadilisha rangi halisi ya picha na kuwa yenye rangi ya mpauko; kama picha za miaka ya nyumawakati kamera zilikuwa hazijafanya maugeuzi katika uboreshwaji wa picha inayopigwa kwenye kamera yenyewe.
Baadhi ya vitu unavyoweza weka kwenye picha
Maboresho hayo ni mazuri na ni jambo la kuvutia kwani sasa unaweza ukaongezea mvuto wa picha au kuharibu kabisa kutokana na kile ulichokiandika au kukichora kwenda kwa mpokeaji wa picha.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post