Utafiti wa Umoja wa Kimataifa (UN) umetoa ripoti inayoonesha uchumi wa Tanzania unanufaika kwa takribani dola milioni 500 za Kimarekani kwa mwaka kutokana na utumiaji wa mfumo wa malipo wa kidigitali.
Bado pato la taifa linapata mchango mdogo sana kutoka kwenye kodi za VAT (Value Added Tax) na utafiti huo unaonesha mapato kutokana na utumizi wa mifumo ya malipo ya kidigitali yanaweza panda hadi dola milioni 477 (Tsh Trilioni 1) kwa mwaka. Utumiaji wa malipo katika mfumo wa kidigitali unasaidia kuzuia upotevu wa pesa kupitia rushwa, utapeli n.k
Matokeo hayo chini ya programu ya
Better Than Cash Alliance ya UN yameonesha sehemu ambazo Tanzania ishanufaika kutokana na utumiaji wa mifumo ya malipo ya kidigitali;
Ukuaji wa mapato katika sekta ya utalii; hii ni kutokana na malipo kufanywa kidigitali (benki, au mifumo ya kibenki ya simu).
Utumiaji huu umeondoa milolongo mirefu (bureaucratic) ya kimalipo na hivyo kusaidia upatikanaji wa huduma kwa haraka zaidi ukilinganisha na zamani; mfano sekta ya bandari imeweza nufaika sana kutokana na kuwawezesha wafanyabiashara kuweza kutoa mizigo yao kwa haraka zaidi ukilinganisha na zamani.
Zamani kufanikisha malipo ya huduma mbalimbali kama vile umeme na maji, leseni za kibiashara mbalimbali n.k zilihusisha taratibu nyingi sana lakini kutokana na ukuaji wa njia bora za kisasa za kidigitali za kufanya malipo (kama vile mobile money n.k) imekuwa ni rahisi sana kukamilisha malipo hayo.
Hili linawasaidia wote, wananchi na serikali. TRA wanaweza kuchukua kodi kwa urahisi zaidi kwa sasa kupitia malipo yanayofanyika kwa kutumia mifumo ya kimalipo ya digitali ukilinganisha na pale ambapo mifumo hiyo hautumiki.
Vifaa kama vya EFD vinavyotumika kwenye biashara mbalimbali katika manunuza ya bidhaa na huduma inasaidia sana pia kuwezesha ongezeko la upatikanaji wa taarifa za malipo ya kodi kwa serikali kwa urahisi.
Je unaona mifumo hii ya kimalipo ya kisasa imekusaidia kwa kiasi gani katika maisha na pilikapilika zako za kila siku?
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon