Jinsi Ya Kujizuia Na Uraibu (Addiction) Wa Kutumia Simu Janja Kila Mara!

Tafiti nyingi zimefanyika na ukweli umegundulika ni kwamba wengi wetu tumepata na uraibu (addiction) juu ya simu janja zetu pengine kuliko vitu vingine.
Kumbuka kuna wengine wanazipenda sana simu zao na hata zikidondoka wao ndio huumia Hahaha! .
Kwa karne hii wengi wanatumia simu janja sana kuliko zile simu zingine (mwanga wa sabuni). Ukaribu wao wa kupitiliza na simu hizo pengine ndio unaosababisha uraibu (addiction) huo.
Katika tafiti iliyofanyika huko British, ilidai ya kwamba katika kila watu watatu (3) basi lazima kuna mmoja ambaye lazima atakuwa anatumia simu yake usiku wa manane.
Sasa kama ukijihisi una uraibu na simu yako nini cha kufanya? Njia ni hii hapa.
1. Weka Simu Yako Mbali Na Ulipo
Ndio! kama simu iko mbali na wewe ulipo hutaweza kuitumia sio? Kuna wengine hapa bado ni changamoto kwani hawawezi kukaa mbali kabisa na simu zao. Lakini kuna wale waliobarikiwa (Kama rafiki yangu, Nasra ) wao wanaweza hata kusahau kabisa walipoweka simu zao mpaka atokee mtu abipu hiyo simu.
2. Futa Baadhi Ya App
Kama unasumbuliwa na uraibu wa simu basi hapo huna budi kufuta baadhi ya App. Na itakua ni vizuri kufuta zile unazozipenda kwani hamu ya kushika simu na kuzifungua mara kwa mara itapungua au itaisha kabisa. Kwa kifupi ni kwamba utashindwa kushika shika simu yako kila mara.
3. Zima Simu Janja Yako
Hivi mara yako ya mwisho kuzima simu yako ni lini? Kuna wengine wanachanganyikiwa kabisa kama simu zao zikizima. Unaweza ukajiwekea katabia ka kuzima simu yako, pengine labda ukiwa bize au ukiwa unalala. Hii kwa kiasi kikubwa itapunguza uraibu kwani hutapoteza muda kupepesa machi katia simu yako hiyo.
4. Jiwekee Muda Maalamu Wa Kutotumia Simu Yako
Wengine wanajiuliza Je, ni kweli inawezekana? Lakini mimi naamini kila kitu kinawezekana. Ukijiwekea muda maalumu ambao hutaweza kugusa simu kabisa itakua ni vizuri na uraibu utapungua kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano unaweza ukajiwekea katabia kwamba kila ifikapo saa mbili usiku hutakua unatumia simu mpaka kesho yake.
5. Usitumie Simu Yako Ndani Ya Dk 30 Za Kwanza Baaya Ya Kuamka
Ukishaamka asubuhi usifanye kuangalia simu yako kuwa ndio kitu cha kwanza kufanya. Fanya vingine vya muhimu unaweza fanya mazoezi pia na ukafanya maandalizi ya kuweza kupata chai. Haya yote yakitumia ndipo unapoweza rudi katika simu janja yako na kujua yale yaliyojiri.
Kama inavyofahamika kuwa uraibu wa aina yoyote ile una kazi sana kama mtu akitaka kuacha hicho kitu ambacho ana uraibu nacho. Hapa cha msingi ni juhudi na dhamira ndiyo itakayo saidia. Kwa Tanzania pengine jambo hili linaweza likachukuliwa Poa! Lakini nina uhakika wapo watu amabao wanasumbuliwa na hili
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini kama kuna njia yeyote ambayo sijaiandika na unahisi inaweza pia ikasaidia.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post