Je ni sahihi kuacha Chaja kwenye Umeme baada ya Kuitumia?

Je chaja ikiwa bado imebakia imechomekwa
huwa inatumia umeme?
> NDIYO!
Ata pale ambapo haujachomeka simu au
kompyuta yako bado umeme unakuwa
unatumika INGAWA ni kiasi kidogo. (Kumbuka
hapa tunamaanisha pia ya kwamba switchi ya
umeme ikiwa ipo imewashwa).
Kwa mfano uchunguzi uliofanywa na mtandao
wa HowToGeek uligundua ya kwamba kama
nyumba ina chaja sita na zote zikawa
zimeachwa kwenye umeme basi kwa mwaka
mzima kuna uwezekano kiasi cha umeme cha
takribani kilowatt (kWh) 2.628 zitakuwa
zimetumika.
Wakati pia utafiti uliofanywa na mwandishi
mmoja wa mtandao wa ZDNet ulitambua ya
kwamba kwa chaja moja ya simu ya iPhone
ikiachwa kwenye umeme kwa kipindi cha
mwaka mmoja itakuwa imetumia kiasi cha
kWh 1.5.
Kwa kifupi haijalishi, kikubwa zaidi ni
kutambua ya kwamba chaja zitaendelea
kunyonya umeme kiasi flani pale zinapoachwa
kwenye umeme.
Inasemekana pia kwa chaja feki na za chini ya
kiwango basi ndio zitatumia umeme mwingi
zaidi.
Inakuwaje chaja iendelee kutumia umeme ata
pale ambapo simu au kompyuta
haijachomekwa?
Chaja zote zina ka’transfoma kadogo ndani
yake. Haka ndio kanakuwa bado
kameunganisha mfumo wa umeme.
Je kuna umuhimu wowote wa kuhakikisha
tunazima au kuchomoa chaja zetu baada ya
kutumia?
> Ndiyo!
Inasemekana kwa nyumba yenye chaja kadhaa
basi uamuzi wa kuzima umeme au kuchomoa
chaja baada ya kutumia zinaweza
kuwahikikishia wanaokoa kiasi flani cha pesa
kila mwaka.
Pia kuacha chaja hizi zikiendelea kupata
umeme kwa muda mrefu ata pale ambapo
hatuzitumii tunazifanywa ziwahi kuchoka ndani
yake na hivyo kuwahi kuharibika ukilinganisha
na kama tungekuwa tunazitumia kiusahihi.
> Pia kuna hatari ya milipuko/shoti ya
umeme!!!!
Hili ni hasa kwa pale chaja za chini ya ubora –
chaja feki, zinapotumika. Chaja za namna hii
kuwepo kwenye umeme kwa muda mrefu kuna
weza sababisha shoti na hivyo kukuweka
wewe na mali zako hatarini.
Soketi iliyoungua kutokana na mtu kuacha
chaja kwa muda mrefu bila kuzima
Ni kitu kidogo tuu, zima switchi ya umeme
baada ya kutumia chaja yako, kama bado hili
ni jambo kubwa basi chomoa tuu.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post