Obama atajua juu ya John Snow kabla yetu.

Raisi wa Marekani Barrack Obama atajua nini kitamtokea John Snow mapema kabla ya mtu yeyote ( Ukiondoa waandaaji wa GOT), hii ni baada ya kuwaomba waandaji wa series hiyo kuona show hiyo kabla haijaanza kuoneshwa. Tamthilia hii huwa inazungumziwa sana mitandaoni.
Game Of Thrones ni tamthilia iliyojipatia umaarufu mkubwa kwa watazamaji wengi, moja ya mambo yaliyoipa tamthilia hii umaarufu ni mtindo wa watunzi wake kubadilisha hadithi kutoka katika hadithi halisi ambayo tamthiliya hiyo iliandikwa.
GOT imekuwa sio kituambacho unaweza kujua nini kitafuata, kila ukiangalia kipande kimoja utataka kuangalia kipande kinachofuata maana hauwezi kutabiri nini kitatokea.
Mhusika John Snow katika tamthilia ya Game of Thrones
Katika toleo lililopita mmoja ya waigizaji wa tamthilia hii ambaye alikuwa anapendwa anayeitwa John Snow alionekana akiuwawa kitu ambacho kiliwahuzunisha wengi wanaoifuatilia tamthilia hiyo (mimi nikiwa mmoja wao) lakini tetesi zinasema kwamba John Snow ataonekana katika toleo lijalo na hii ndiyoimezidisha hamu ya kutaka kujua kilichomo katika toleo lijalo.
Waandaaji wa tamthilia hii wamekuwa ni wa siri wakubwa katika uandaaji wa tamthilia hii kitu ambacho kinapelekea watu wengi kutojua nini kitakuja kutokea katika toleo linalofata la GOT.
Hata hivyo waandaji hao wamesema kwamba raisi wa Marekani amewaomba kuona tamthilia hiyo mapema zaidi na wao wamemkubalia hivyo kumfanya mtu peke ambaye siyo muandaaji ambaye atajua mwisho wa John Snow kabla ya watu wengine wote.
Tamthilia hii itaanza kuonesha sehemu ya 6 hapo tarehe 24 mwezi wa huu na itakuwa ikioneshwa katika televisheni ya marekani ya HBO.
Vipi unafuatilia tamthilia hii? tuambie nini unazani kitamtokea John Snow, Je amekufa kweli? atakuja kama wafu? ama atakuwa hakufa alipopigwa mapanga?.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post