Njia 5 Za Kupata Ujazo Wa Uhifadhi Katika Kompyuta Yako!

Hata katika kompyuta zetu ujazo siku hizi hautoshi, haijalishi hata kama una GB 500 za ujazo. Mambo yamekuwa mengi siku hizi na vitu vingi tunavyovipenda tunaamua kuvihifadhi.
Kwa kutumia huduma za kuhifadhi vitu kwa mtandao unaweza ukahifadhi mafaili mengi sana mtandaoni. Lakini kumbuka mafaili mengi tunayoyahifadhi huko mengi ni yale ambayo yana ujazo mdogo.
Kompyuta Ambayo Ujazo Wa Uhifadhi Wake Umejaa
Kwa mafaili yenye ujazo mkubwa punda wetu wa kumbebesha inakua ni kompyuta zetu. Pale ujazo huo unapokaribia kujaa ndio tunapoanza kuangalia kipi tunakipenda na kipi hatukipendi na kukifuta.
ITphide leo inakujuza njia kadhaa za kuweza kujipatia uhifadhi wa ziada katika kompyuta yako kwa kutumia ujanja huu.
1. Futa mafaili katika ‘Recycle Bin’. Mafaili ambayo umeyafuta na yakaingia katika ‘recycle bin’ bado yanakula nafasi hivyo inabidi kuyafuta kabisa
2. Tumia ‘Disk Cleanup’ nenda kwenye Start>>All Apps>>Windows Administrative Tools>>Disk Cleanup kisha fungua ‘Disk Cleanup’
3. Tumia njia ya nje katika kuhifadhi mafaili yako. Njia ya nje inaweza ikawa kama vile kutumia ‘Hard Disk’ ya nje.
4. Futa App na Programu ambazo hazihitajiki au hazitumiki kwa wakati huo au kwa kipindi cha karibuni. Hii itakusaidia kuongeza ujazo wa uhifadhi. Kama ukijisikia unataka kuitumia App au programu unaweza ukaipakua kwa mara nyingine. Kufanya hivyo nenda katika ‘Control pannel’ ya kompyuta yako na uanze kupunguza baadhi ya programu
5. Hifadhi vitu katika mtandao. Unaweza ukahifadhi vitu kama vile picha, miziki n.k katika mtandao (Cloud). Japokuwa mtandao unachukua vitu venye uhifadhi mdogo, kizuri ni kwamba huduma za kuhifadhi kwa mtandao ziko nyingi na kwa sababu hiyo unaweza kuamua kuhifadhi mambo mengi tofauti tofauti kwa mtandao zaidi ya mmoja.
Kitu cha nyongeza ni kwamba usiwe unapenda ku ‘Hibernate’ kompyuta yako. Teknolojia ambayo iko nyuma ya jambo hili ni mfano kama wewe unavyopiga ‘Screenshot’ kitu. Hivyo hvyo kompyuta inafanya na kuhifadhi hali ambayo kompyuta iko nayo ili utakapokuja kuanza kutumia tena utaikutia pale pale. Jambo hili – wachache sana wanalijua — linajaza nafasi

Previous
Next Post »

Ads Inside Post