Madhara ya kulala na Simu yako ikiwa Imewashwa

Wengi wetu tumekuwa ni watumiaji wazuri wa simu zetu pengine hata kufikia kulala nazo kitandani ama tukitaka tusipitwe na simu fulani ya muhimu ama kwa sababu tunapitiwa na usingizi wakati bado tunachati.
Tabia hii sio salama kwa afya na usalama wetu, makala hii itakusaidia kuelewa madhara yaliyopo iwapo unalala na simu yako ikiwa imewashwa.
Jambo la kwanza ni kwamba simu kama kifaa cha kielektroniki inaweza kusababisha shoti ya umeme muda wowote hasa ikiwa inachajiwa, hili linzweza kusambabisha madhara mengi ikiwamo lile la moto. Pia kwa bahati mbaya wengi wetu huwa hatusomi maelezo ya jinsi ya kutumia simu zetu na mara nyingi kuna matumizi ya chaja zisizokuwa rasmi na zilizochini ya ubora…na muda mwingine ata betri za simu zinazonunuliwa muda wa kubadilisha zinakuwa zilizochini ya kiwango.
Kulala na simu ni Hatari : Simu janja ikiwa imeungua baada ya kuwekwa chini ya mto. Picha kwa hisani ya mtandao
Jambo la pili ni kwamba kwa kutumia simu kitandani kuna uwezekano mkubwa sana ukaharibu mfumo wako wa usingizi, ingawa wengi wetu hatujali sana hili lakini ni kweli kwamba ufanisi wako wakati wa mchana unategemea hasa ulilalaje wakati wa usiku. Mwanga unaotokana na simu yako unasifika kwa kubadili namna ambayo wewe ulikuwa unalala na mwanga huu hukufanya usilale na kupumzika vizuri.
Inaaminika kwamba simu zinatoa mionzi ambayo inaweza kusababisha kansa, ingawa hili bado limewagawanywa watafiti lakini hata shirika la afya duniani limeisha waonya watu dhidi ya madhara hayo ambayo bado yanachunguzwa. Watafiti bado wanaendelea kufanya uchunguzi ila kuna tafiti mbalimbali zinakuja na matokeo tofauti – wengine wakisema hakuna uhusiano kati ya utumiaji simu na kansa huku wengine wakisema uhusiano upo ila ni mdogo na madhara ya utumiaji yanatokea miaka mingi sana baadae. Hapa tunakuachia wewe – ila ushauri mzuri ni BORA KINGA… – Vyanzo
NYDailyNews , na Cancer.Gov
Teknokona inakushauri kutumia earphones kusikiliza simu ambazo zinazidi dakika ishirini na kama una mtoto mdogo usiruhusu kabisa asikilize simu wala kuchezea simu maana fuvu la kichwa chake bado ni changa hivyo ni rahisi zaidi kwake kuathirika ukilinganisha na watu wazima.
Soma Pia – Mambo 6 Yasiyo ya Kweli kuhusu Kuchaji Simu
Endelea kutembelea mtandao wako wa itphidel.logspot.com kwa habari za teknolojia kwa lugha ya kiswahili.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post