Intruder Alarm System; Fahamu kuhusu mfumo wa Ulinzi na Usalama na Nickson  7 dakika ny

Intruder Alarm System ni mfumo wa ulinzi ambao unatumika kuzuia wezi katika nyumba au katika sehemu ya biashara. Mfumo huu unatumia vifaa maalumu amabavyo vinaweza kugundua uwepo wa mtu katika eneo husika na hupiga king’ora na pia huweza kutuma meseji kwa mtumiaji kumjulisha juu ya tukio husika.
Makala hii ni mwendelezo wa makala zinazohusu teknolojia zilizopo za usalama wa majumbani kwetu, tumekwisha ona kwa muhtasari upande wa CCTV hivyo makala hii tutaangalia kwa muhtasari juu ya Intruder Alarm system mfumo ambao unatumika zaidi katika maofisi na majumbani kuzuia wezi kuingia nyakati ofisi/nyumba hazina watu.
Mfumo huu wa Intruder alarm system unakuwa na vifaa vikuu vya aina tatu ambavyo ni Panel, detector, keypad pamoja na ving’ora.
Panel la Intruder alarm system likiwa na keypad yake
Panel hichi ndio kama kichwa cha mtambo, panel hupokea taarifa kutoka katika detector juu ya uwepo wa mtu yeyote katika eneo ambalo detector hiyo ipo pia panel inakuwa imeungwa na ving’ora kwaajiri ya kuwacha vifaa hivyo wakati wa tukio la wizi. Tofauti ya intruder alarm system na CCTV system ni kwamba intruder alarm ina uwezo wa kumsumbua mwizi pindi anapokuwa katika eneo la tukio kwa kupiga kelele.
Moja ya aina ya detector ambayo ni mahususi ya sehemu za nje ya nyumba.
Detector ni vifaa ambavyo vinahusika katika kuangalia kama kuna movement yeyote ya binadamu katika eneo husika, kifaa hiki kinatumia teknolojia ya infrared detection ambayo inakisaidia kuweza kugundua movement yeyote inayotokea katika eneo husika. Vifaa hivi vipo vya katika aina mbali mbali inategemea na mahitaji yako.
Keypad ni kifaa muhimu katika mtambo huu kwani ndicho kinachotumika sio tu kuprogram bali hata ku washa na kuzima mtambo wako pindi unapoingina na kutoka nyumbani.
Keypad
Ving’ora vinawakilisha kundi la vifaa vyote ambavyo vinapokea amri kutoka katika panel, baada ya kupewa amri ya kufanya kazi hasa baada ya panel kupokea taarifa ya movement katika eneo fulani basi kingora hupiga kelele ambazo zinalenga kuwajulisha wamiliki wa mali kwamba kuna mtu ameingia katika eneo lao.
king’ora ambacho kinatumika kupiga kelele wakati wa tukio la wizi
Yapo makampuni mengi ambayo yanafunga mitambo kama hii katika majumba na katika offisi na pia wapo mafundi binafsi ambao wanaweza kufunga na kufanya programming ya mitambo hii.
Intruder Alarm system inazifaa familia ambazo hazina walinzi nyumbani ama zile ambazo hazina wafanyakazi ambao wanaweza kubaki na kulinda nyumba nyakati ambazo nyumbani hakuna mtu, kwa familia kama hizi ambazo hazina huduma ya walinzi ama hazina mtu ambaye anabaki nyumbani zinahitaji mitambo kama hii ifungwe nyumbani ili wakati hamna mtu ama wakati wa usiku itoe msaada wa ulinzi.
Endelea kufuatilia Teknokona nasi tutaendelea kukuletea makala za teknolojia zinazo weza kukusaidia katika maisha yako.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post