Kuwa Makini ‘Emoji’ Moja Inaweza Kutofautiana Kati Ya Simu Na Simu!

Japokuwa Emoji zinasaidia kwa kiasi kikubwa kwenye kunogesha na kuweka mbwembwe kadhaa katika ujumbe bado unaweza shangaa mtu unaemtumia ujumbe huyo akakuelwa tofauti kabisa kutokana na Emoji hiyo.
Muda mwingine Emoji zinaziba mapengo katika maeneo ambayo hatuwezi kuweka maneneno ya kawaida kabisa. Wana teknolojia walivyoliona hilo wakaboresha Emoji kwa kuziboresha na kuongeza zingine ambazo hazipo au zilikuwa zinakosekana. Moja kati ya maboresho makubwa yaliyofanyika ni kama vile kuweka Emoji za rangi zikiwa ziko kama kioo cha rangi kwa wale watu wanaozituma au wanaotumiana Emoji hizo.
Watafiti wamegundua kuwa kwa kiasi kikubwa Emoji zinatofautiana katika programu endeshaji mbalimbali. Mambo makubwa yananoyotofautiana ni kwenye mashavu, nyusi zao, hii inamaanisha kuwa unaweza ukamtumia mtu Emoji yenye bonge la tabasamu kutoka katika simu yako lakini yeye kule akaipokea kama tabasamu la kawaida tuu (tabasamu dogo)
Japokuwa kwa kiasi kikubwa Emoji hizo ambazo zilikuwa zikitofautiana kutoka kwenye kifaa kimoja hadi kingine ni kwamba zilikuwa hazibadilishi maana kabisa. Kwa kiasi kidogo sana ndio zilikuwa zinaweza kubadilisha maana na kuzalisha maana mpya.
Hapa kuna aina tofauti tofauti za vifaa kama vile Apple, Samsung na LG na hata Google ambapo wanaonyesha Emoji moja lakini ikiwa na muonekano tofauti kabisa katika vifaa hivyo.
Emoji Moja Lakini Ikiwa Na Muonekano Tofauti Katika Vifaa
Hapa cha kufanya ni kuwalaumu watengenezaji wa wa vifaa ambao wamevuka kabisa mipaka ambayo imewekwa na Unicode (watengenezaji wa Emoji). Mipaka ambayo Unicode waliiweka ndio ambayo ingefanya Emoji zote kuwa za aina moja.
Sasa siku hizi makampuni ya simu yanabadilisha simu karibia kila mwaka na programu endesha ji (OS) zao pia wanazibadilisha. Jambo hili linawafanya waboreshe mambo mengi katika vifaa vyao hivyo, kwa kufanya hivyo wanajikuta wanaingia mpaka kuboresha Emoji hizo alafu wanapitiliza
Emoji Nyingi Na Muonekano Wake Kwa Vifaa Tofauti Tofauti
Kama unahisi unaweza kumchanganya mtu ambae unamtumia Emoji, unaweza tuu ukazima kutumia Emoji katika kifaa chako. Baada ya hapo utakuwa unatumia njia za kawaida katika kutuma na kupokea ujumbe.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post