Bastola Inayokunjika na kuchukua muonekano wa Simu-Janja, Ukaificha mfukoni!

Kampuni inayoitwa Ideal Conceal imetengeneza bidhaa yake ya kwanza, bunduki a mkononi inayoweza kukunjwa na kuonekana kama simu-janja ndani ya kasha yake (kava). Pistol hiyo ni ya .368 na inajikamata kisawasawa iwapo imefunguliwa, kufanya isichezecheze.
Ukiifunga, sehemu ya kufyatua risasi inafichwa barabara na mkono wako, na hivyo kuonekana kama simu-janja. Pia, kipo hata kishikio cha bunduki hiyo cha kiunoni chenye muonekano wa kishikio cha smu-janja.
Bastola Inayokunjika na kuchukua muonekano wa Simu-Janja
Simu hiyo ya kijanja itapatikana nchini Marekani. Kwa sasa na kwa maana nzuri zipo sheria zilizopitishwa na maeneo husika (majimbo) kuzuia au kudhibiti silaha zenye mfumo wa kufichika.
Tovuti ya yahoo.com inakariri meneo ya kwenye tovuti ya kampuni ya Conceal yanayosema kwamba, “Wazo la Ideal Conceal linaendana na ongezeko la mahitaji ya bunduki ambazo watu wanaweza kubeba kirahisi kila siku. Kuanzia wakina-mama wa nyumbani na hata watu wa kazi maalumu za kila aina , hii bunduki inakupa chaguo la kutokuwa mhanga.”
Kwa muda huu, pistol hizi bado ziko matengenezoni na hazijatolewa kwa ajili ya mauzo, hatahivyo, kampuni ya Ideal Conceal inategemea kuanza kuziuza katikati ya mwaka 2016. Kupitia mahojiano na
CNNMoney , imejulikana kwamba mmiliki wa kampuni, Kirk Kjellberg amepokea barua pepe 2,500 kutoka kwa watu wanaotaka kununua silaha hiyo.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post