Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro inakabiliwa
na upungufu wa walimu 200 wa masomo ya
sayansi katika shule za sekondari hali ambayo
imesababisha wanafunzi kushindwa kufanya
vizuri kitaaluma na hivyo kuisababisha wilaya
hiyo kushika nafasi ya mwisho kimkoa.
Afisa elimu sekondari wilaya ya Same Bi
Happynes Laizer amesema walimu wengi
wanaopangiwa kufanya kazi katika wilaya hiyo
wamekuwa hawaripoti kutokana na jiografia ya
wilaya hiyo kuwa na milima.
Amesema wanafunzi wengi wanakata tamaa
kutokana na ukosefu wa walimu, wanafunzi
kutembea umbali mrefu na ukosefu wa vifaa vya
kufundishia hali ambayo inasababisha kiwango
cha taaluma katika wilaya hiyo kuzidi kushuka
kila mwaka.
Walimu wanasema wanafunzi walio wengi
hawana utamaduni wa kujisomea kutokana na
wilaya hiyo kutokuwa na maktaba, pamoja na
ukosefu wa vitabu vya kutosha mashuleni hali
inayochangia wanafunzi wengi kushindwa
kufanya vizuri kitaaluma.
Nao baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari
ya Kwakoko wilayani Same ambao wamepatiwa
kompyuta ndogo za mkononi zenye vitabu vya
kujifunzia wanasema kwa sasa wana uhakika wa
kufanya vizuri kitaaluma.
Uncategories
Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro
inakabiliwa na uhaba wa walimu 200 wa
masomo ya sayansi.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon