Wananchi waitaka serikali kuyarudisha matangazo ya bunge kupitia TBC:

Wakazi wa mkoa wa Morogoro wamesisitiza
Serikali kurudisha utaratibu wa kuonesha
moja kwa moja matangazo yote ya Vikao
vya Bunge ili waweze kuona wanachofanya
wawakilishi wao waliowapa Dhamana ya
kuwawakilisha Bungeni.
Wakizungumza na star tv kwa nyakati
tofauti mjini Morogoro Wananchi hao
wamesema hawakubaliani na utaratibu wa
serikali wa kuamua TBC kurusha moja kwa
moja sehemu ya Maswali na majibu na
baada ya hapo kurekodiwa na kurushwa
usiku.
Wamebainisha kuwa pamoja na stesheni
zingine za televisheni ikiwepo Star tv
kurusha matangazo hayo, ,lakini wananchi
wana haki ya kuangalia televisheni yao ya
taifa kwa kuwa inaendeshwa kwa kodi za
watanzania .
Uamuzi wa serikali wa kusitisha matangazo
ya moja kwa moja bungeni baada tu ya
kipindi cha maswali na majibu kumendelea
kuleta simtofahamu kwa wanachi walio
wengi , ambapo mkoani, Morogoro uamuzi
huo umepokelewa kwa hisia tofauti.
Wakazi wa mkoani hapo wanaona kufanya
hivyo ni kutaka kuwakosesha haki ya
msingi ya kupata habari kwa kuona nini
wanacho kifanya wawakilishi wao
waliowatuma .
Serikali ilitoa mapendekezo hayo ikidai
kupunguza Gharama zinazo tumika kurusha
matangazo hayo ambapo zaidi ya Bilion 4
hutumika kwa mwaka, huku ikielezakuwa
zaidi ya asilimia 80 ya watanzania
hawaangalii matangazo hayo muda wa
mchana.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post