Wananchi Shinyanga waitaka mahakama kutoa elimu ya kisheria kwa jamii haswa vijijini ili kupunguza migogoro ya ardhi.

Serikali imeshauriwa kuweka mpango mkakati wa
kutoa elemu ya kisheria kwa wananchi kwakuwa
uelewa mdogo na kutoelewa tafsiri ya kisheria
inasababisha wananchi kulalamikia mfumo wa
mahakama katika kutoa hukumu na kudai
kutokutendeka haki wakati wa kutolewa hukumu
hizo.
Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi wa
mkoa wa Shinyanga wakati wa ufunguzi wa wiki
ya sheria ambapo wananchi hao wameitaka
serikali itafute njia ya kufikisha elimu juu ya
tafsiri ya sheria haswa katika maeneo ya vijijini
ambapo kwa wakati huu kumeibuka migogoro
mingi ya ardhi inayosababishwa na uelewa
mdogo wa sheria.
Aidha hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya
Shinyanga Bw. Denis Luhungo amedai kuwa
kwakuanzia mahakama imeanza kutoa elimu juu
ya mfumo wa sheria kwa wananchi kupitia
vyombo mbalimbali vya habari huku naibu msajili
mahakama kuu kanda ya Shinyanga Bi. Sekela
Mwaiseje akidai kuwa maonyesho ya wiki ya
sheria yanalenga kutoa elimu ya kisheria kwa
wananchi wote ambapo vyombo vyote vya dola
ikiwemo Takukuru, polisi na mahakama yenyewe
wamejipanga kutoa elimu hiyo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Bi. Josephine Matiro ameiomba mahakama
kuweka mpango endelevu kutoa elimu ya kisheria
kwa wananchi isiishie katika wiki ya sheria pekee
kwakuwa kuna malalamiko mengi ya wananchi
wakidai kutotendewa haki katika mambo ya

Previous
Next Post »

Ads Inside Post