Wabunge wa mkoa wa Mara wameonesha
kusikitishwa kwa kiasi kikubwa na kitendo cha
uongozi wa hifadhi ya taifa ya Serengeti
kushindwa kuchangia fedhwa kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya imaendeleo
katika vijiji vinavyozunguka hifadhi hilo huku
wakidai miradi hiyo imekuwa kutolewa kwa
ubaguzi hatua ambayo wamesema imechangia
kuongeza chuki kati ya wananchi na wahifadhi.
Wakizungumza katika kikao cha ushauri cha
mkoa RCC mkoani Mara wabunge hao kwa umoja
wao, wamesema licha ya eneo kubwa la hifadhi
ya taifa ya Serengeti kuwa mkoa wa Mara, lakini
wananchi wake wameshindwa kunufaika na
hifadhi hiyo ukilinganisha na mikoa mingine.
Hata hivyo mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya
Serengeti Bw William Mwakilema, akizungumza
katika kikao hicho amesema hifadhi hiyo
imekuwa ikichangia huduma za jamii katika vijiji
vinavyozunguka hifadhi yake lakini pia kuchangia
pato la taifa.
Wilaya za mkoa wa Mara zinazopakana na
hifadhi hiyo ya taifa ya Serengeti ni pamoja
wilaya ya Serengeti, Bunda na Tarime.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon