Jeshila polisi limelazimika kutumia mabomu ya
machozi kuwatawanya wananchi zaidi ya 30
waliovamia kituo cha polisi duthumi kata ya
Bwakila chini wilayani Morogoro waliokuwa na
silaha za jadi, ambao wamevunja mlango
mkubwa wa kituo hicho kwa nia ya kuwakomboa
wenzao watatu,waliokuwa wamekamatwa
wakituhumiwa kuhusika na wizi wa mifugo.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro
Grifton Mushi, amethibitisha kutokea kwa vurugu
hizo na kwamba wanawashikilia watu watatu
zaidi kuhusiana na tukio hilo ambapo amedai
kundi hilo la wananchi wakiwa na silaha za jadi
ikiwemo mashoka,mapanga na
marungu,walivamia kituo hicho cha polisi
Duthumi kwa nia ya kuwakomboa wenzao
waliokuwa wamekamatwa kwa tuhuma za wizi
wa mifugo ya teu saningo,mkazi wa Bwakila
chini,ambapo hata hivyo tayari watuhumiwa hao
walikuwa wameshahamishwa.
Taarifa zaidi kutoka eneo la tukio zimedai kuwa
awali wananchi walikuwa wameikamata mifugo
hiyo wakituhumu kula mazao kwenye mashamba
lakini wakati wakiilinda walimchinja mmoja na
kumla, jambo lililofanya polisi kuwakamata
waliohusika,ndipo kiongozi mmoja wa kisiasa
akadaiwa kuwakusanya wananchi na kuwahimiza
wakawakomboe wenzao,ndipo zilipozuka vurugu
hizo.
Mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo
akizungumza kwa njia ya simu kutoka
duthumi,ameeleza kushangazwa na hatua ya
polisi kuachana na kesi ya msingi ya mifugo kula
mazao,badala yake kuigeuza kuwa ya wizi wa
mifugo,huku mfugaji aliyelisha mazao
mashambani akiachwa huru,na kwamba katika
kuwatawanya,polisi wametumia silaha za moto
zilizojeruhi baadhi ya watu waliokwenda
kuwawekea dhamana wenzao.
Katika tukio jingine,wananchi wa kitongoji cha
mizizini, kijiji cha Maseyu, wamechoma mabanda
manne na vifaa vya uchimbaji madini, mali ya
ayubu bishangazi, na kumjeruhi mwekezaji huyo ,
wakimtuhumu kutumia kemikali za sumu
kusafisha madini,ambapo polisi inamshikilia mtu
mmoja kuhusika na tukio hilo.
Baadhi ya wananchi wa morogoro wamelaani
kitendo cha baadhi ya watu wanaojichukulia
sheria mikononi,pindi wanapotafuta haki,ingawa
wengine wakadai kitendo cha kukamatwa kwa
watuhumiwa na kuachiwa au kutochukuliwa
hatua kimewafanya wananchi kukosa imani na
serikali yao hususani vyombo vya dola na
kuamua kujichukulia sheria mikononi.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon