Ujambazi Kimara Temboni

YALIYOJIRI Watu wanaodaiwa kuwa majambazi
wamevamia maduka matano katika mtaa wa
Kimara Temboni, Kinondoni, jijini Dar es Salaam
na kupora fedha na mali mbalimbali pamoja na
kujehuri watu wawili kwa risasi. Tukio hilo
lilitokea usiku wa kuamkia jana, wakati
majambazi hao walipovamia eneo hilo wakiwa
katika pikipiki mbili na gari mbili, huku
wakiwataka wateja na wauzaji waliokuwa katika
maduka hayo kulala chini.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post