Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali
imesababisha wananchi 61 wa kata ya
Kwanyama wilaya Tandaimba mkoani Mtwara
kukosa makazi baada ya nyumba zao kubomoka
na zingine kuezuliwa mapaa na kusababisha
baadhi ya kaya kuharibu chakula.
Akizungumzia tukio hilo diwani wa kata ya
Kwanyama Mohamed Issu amesema mvua hiyo
imeleta athari kutokana na baadhi yao kuumia,
kupoteza vyakula, majengo ya shule ya
Kwanyama kuezuka paa, huku waathirika
wakielezea tukio hilo lilivyotokea.
Kwa mujibu wa kitengo cha maafa cha wilaya
hiyo nyumba zilizoathirika ni 61 na kimelazimika
kutoa msaada wa chakula, huku mbunge wa
jimbo la Tandaimba Ahamadi Katani naye
akalazimika kutoa bati miatatu.
Baadhi ya wahanga wa tukio hilo wameishukuru
serikali, na mbunge wao kuwajali kwa tukio hilo,
na wameendelea kuomba wadau wengine
kuwasaidia ili warudi katika maisha ya kawaida
ikiwa ni pamoja na watoto kwenda shule ambao
kwa sasa hawaendi.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon