Bunge latengua kanuni

Akitengua kanuni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Walemavu katika Serikali ya
Awamu ya Tano, Jenista Mhagama amesema
kwamba bunge lilitakiwa likae kama kamati
mwezi Nombemba ili liweze kujadili mpango wa
serikali lakini kutokana na uchaguzi mkuu
uliokuwepo nchini kazi hiyo ilishindikana.
Kwa msingi huo kutokana na uwezo wa bunge
kupitia ibara ya 63 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inayowezesha bunge
kujadili mipango ya serikali,kwa muda muafaka
serikali imeamua kutengua kanuni ili bunge likae
kama kamati kwa muda wa siku 5 ili kujadili
mpango wa serikali ili wabunge waweze kuishauri
serikali kabla ya bunge la bajeti.
Aidha mpango huo ulishindwa kujadiliwa bungeni
hapo juzi kutokana na kanuni za bunge kukiukwa
kwa kusomwa bila kutengua kanuni ya 94(1).

Previous
Next Post »

Ads Inside Post