Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini Joseph
Msukuma Kasheku (CCM) ameiomba serikali
kufanya utafiti wa kina kati ya madawa ya
kulevya ya mirungi,bhangi na pombe za
makaratasi maarufu kama viroba nini kina
madhara zaidi kwa vijana. Mbunge huyo ameyasema hayo katika kikao cha
5 cha bunge la 11 linaoendelea na vikao vyake
katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
''Mheshimiwa mwenyekiti zao la mirungi na
bhangi kuna nchi zinaruhusu mfano majirani zetu
wa Kenya ndege mbili kubwa hutua nchini humo
kuchukua mirungi na kupeleka ulaya sasa kwa
nini sisi tusiendeleze zao hili linalopatikana Geita
na maeneoya Bunda mkoani Mara na maeneo
mengine nchini ili wananchi wanufaike kwa
kuuza zao hilo lakini nchi ipate fedha za kigeni
pia''
Msukuma ameongeza kuwa ''kwa wasukuma kule
kwetu mtu akitumia bhangi analima sana hata
hekari mbili lakini inakatazwa na wakati huo huo
vijana hawa wanadhoofika kwa viroba hivyo
tufanye utafiti ili kama viroba ndivyo vyenye
athari zaidi vipigwe marufuku.
Wakati huo huo Naibu Waziri Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto katika Dkt Khamis Kigwangalla
amesema madawa ya kulevya ya bhangi na
mirungi yana athari kubwa sana za kiafya na
hasa afya ya ubongo na serikali kwa namna
yoyote haitakubali kuruhusu au kujadili kwa
namna yoyote kuhalalishwa kwa madawa hayo.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon