Je betri za simu huwa zinalipuka? Ndio, huwa
inatokea na huwa inaweza kusababishwa na
mambo mbalimbali, leo fahamu ni nini hasa
cha kufanya kuepuka jambo ili kutokea.
Kumbuka kusambaza makala hii kwa ndugu
na marafiki ili nao waweze kuwa salama siku
zote pale wanapofanya maamuzi ya kununua
simu au pale wanapotumia simu zao.
Kitu cha kukumbuka ni kwamba kwa kiasi
kikubwa betri za simu siku hizi
zinatengenezwa chini ya uangalizi mkubwa na
wa kiteknolojia ya juu. Mara nyingi pale
zinapokuwa na tatizo mara nyingi huwa kwa
sababu ya kutumia betri au chaja
zilizotengenezwa chini ya viwango na
makampuni yasiyo rasmi, na ata pale
inapokuwa imetokea nje ya sababu hii basi
itakuwa imesababishwa na sababu zingine
zisizo za kikawaida.
>Hakikisha unanunua simu au betri zenye
ubora/kiwango cha juu.
Hakikisha unanunua simu iliyo kwenye kiwango
na ubora salama. Je ni simu kutoka kwenye
kampuni inayoaminika? Pia angalia kama ni
‘original’ kwani kuna makampuni mengi kutoka
Uchina huwa yanaiga umbo na vitu vingine
mbalimbali vya simu maarufu duniani na
kuzitengeneza zikiwa chini ya viwango. Simu
zilizochini ya viwango kutoka makampuni ya
simu yasiyoeleweka ni hatari kwako. Na rudia
tena, NI HATARI SANA KWAKO!
Utumiaji wa chaji zisizorasmi ukiwa
umeharibu simu ya Samsung
Pia angalia kama betri katika simu yako
imeandikwa taarifa muhimu zinazofanana na
chaja iliyoambatanishwa nayo. Usikubali
kununua betri lisilokuwa na maandishi yeyote
yale, mfano ya taarifa za volti (voltage)
inayotumia ambayo inatakiwa kuwa sawa na
iliyo kwenye chaja yake.
>Usiache simu yako katika mazingira ya joto
sana!
Upo jikoni? weka simu yako mbali na joto kali,
pia ata kama ni nje usiiache kwenye miale ya
jua kali kwa muda mrefu. Joto hili linaweza
sababisha mlipuko wa betri husika, na ata
kama haitalipuka muda huo basi ujue
unaharibu ubora wake.
>Ukiwa unaichaji!
Hakikisha ipo mbali na eneo lenye joto kali.
Pia kama inakubidi upokee au upige simu basi
ichomoe kutoka kwenye chaji.
>Usiku!
Hatari za kulala na simu inayochajiwa usiku
kucha kitandani
Hakikisha unaweka simu yako umbali kidogo
kutoka unapolala, mfano weka kwenye stuli au
meza iliyo pembeni ya kitanda chako. Usilale
na simu kitandani, kwa sababu hii itamaanisha
itakuwa karibu na eneo la kichwa chako, hii ni
hatari sana kwani kama kutakuwa na kitu
ambacho hakiko sawa katika simu hiyo na
kuifanya ilipuke basi utakuwa kwenye hatari
sana. Wengine huwa wanachaji simu usiku
kucha huku wakiiweka simu hiyo kitandani
pamoja nao, hili ni jambo la hatari.
>Uwe unaipa muda simu kupoa baada ya
matumizi mazito na ikapata joto kali!
Ndio mara nyingine utakuta ni wewe ndiye
umeitumia simu muda mrefu bila kuipumzisha
na ata simu hiyo ikaanza kupata joto kali,
ikitokea simu yako imeshika joto sana iweke
sehemu ipate kupoa na ndiyo uitumie tena.
Je uchaji simu yako ikiwa na kiwango gani
kuzidi kuifanya betri iwe kwenye ubora mzuri?
Watafiti wanakushauri kama betri ya simu
yako ni ya ‘Li-ion’ hakikisha mara nyingi
inakuwa na chaji zaidi ya asilimia 50, mara
nyingi betri za simu hizi zinakuwa zinaharibika
kama zinakuwa zinakuwa chaji ndogo mara
kwa mara.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon