ACT-Wazalendo
TAARIFA KWA UMMA:
Tumekuwa tukipokea simu za waandishi
mbali mbali baada ya kauli ya jana ya
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC),Jecha Salum Jecha kuwa hakuna
chama kilichojitoa katika uchaguzi
unaotarajiwa kufanyika machi 20 mwaka huu
Msimamo wa ACT-Wazalendo ni kuwa
hatutashiriki Uchaguzi huo kama
ilivyoazimiwa katika kikao cha kamati kuu
cha february 14 mwaka huu
Hatushiriki kwa kuwa tunaamini kuwa
hakuna sababu ya kufanyika uchaguzi
mwingine nje ya ule uliofanyika Oktoba 25
mwaka jana
Taarifa hii ya kutoshiriki uchaguzi wa machi
20 mwaka huu imewasilishwa katika ofisi ya
ZEC Zanzibar february 9 mwaka huu baada
ya wao kututaka tuthibitishe kwa maandishi
kama tutashiriki au la
Hivyo kauli ya Jecha kuwa hakuna chama
kilichofuata utaratibu ni muendelezo
mwingine wa kutaka kuhalalisha haramu
kuwa halali kama walivyofanya katika kufuta
uchaguzi wa Oktoba 25
Kwa kuthibitisha dhamira yetu hii ya
kutoshiriki hivi karibuni kamati Maalum ya
uongozi Zanzibar ilimsimamisha uanachama
ndugu Khamis Idi Lila,aliyedhaminiwa na
chama kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar
katika uchaguzi uliofutwa kwa "Zengwe"
hivyo hatuna mwanachama anayewania
nafasi hiyo
Jecha amezungumzia Sheria ya Uchaguzi na
wajibu wa mgombea aliyedhaminiwa na
chama kuthibitisha ushiriki wake,huku
akiacha kwa makusudi kuainisha udhamini
huo ni katika uchaguzi gani
ACT-Wazalendo haijamdhamini
mwanachama wake yeyote kwa ajili ya
kushiriki uchaguzi wa Machi 20 na hili
lilipewa msisitizo katika kikao cha kamati
kuu iliyofanyika february 14 na taarifa
kutolewa kwa umma siku iliyofuata
Tunaomba wananchi wapuuze ulazimishaji
huu wa ZEC kwa kutaka kuionesha dunia
kuwa vyama vimeshiriki uchaguzi huo
haramu
ACT wazalendo katika kikao chake cha
kamati kuu iliazimia kuwa haitakuwa muhuri
wa kuwasafisha wabakaji wa Demokrasia
kwa kushiriki uchaguzi wa Machi 20
Abdallah Khamis
Afisa Habari
ACT Wazalendo
Uncategories
ACT-Wazalendo Watoa Msimamo wao
Baada ya Jecha Kusema Hakuna
Chama Kilichojitoa Uchaguzi
Zanzibar...
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon