Watu 3 wamefariki dunia baada ya Noah kugongana uso kwa uso na basi la Adventure Dodoma.

Watu watatu wamefariki dunia papo hapo baada
ya gari aina ya toyota Noah yenye namba za
usajili T243 DGB lililokuwa likitokea jijini Dar es
Salaam kuelekea mkoani Tabora kugongana uso
kwa uso na basi la abiria la kampuni ya
Adventure lenye namba za usajili T 852 CBF
lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kuelekea jijini
Dar es Salaam katika kijiji cha Buingiri madukani
wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 9 alasiri
ambapo kwa mujibu wa mashuhuda na abiria
waliokuwa ndani ya basi wanasema ajali hiyo
imetokana na mwendokasi wa gari aina ya Noah
ambalo dereva wake alipoteza mwelekeo na
kisha gari hilo kuhama na kulivaa basi na watu
watatu kupoteza maisha papo hapo huku mmoja
akijeruhiwa vibara.
Muda mfupi baada ya kutokea kwa ajali hiyo
jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Dodoma
lilifika eneo hilo na kukuta msongamano mkubwa
wa magari kutokana na ajali hiyo kuziba eneo la
barabara hali iliyowalazimu kuyaondoa magari
hayo ili kuruhusu shughuli zingine kuendelea.
kwa upande wake kamanda wa polsi mkoa wa
Dodoma David Misime akizungumza katika eneo
la tukuio amewataja miongoni mwa watu
waliofariki dunia ni dereva wa Noah
aliyetambulika kwa jina la Abdalah Said Hajiru
mkazi wa Dar es Salaam huku maiti nyingine
mbili zikishindwa kutambulika mara moja ambapo
pia jeshi hilo limefanya jitihada za kuwatafutia
basi lingine abiria na tayari wameendelea na
safari yao.
Awali kabla ya vikosi vya usalama kufika eneo
hilo wananchi wenye hasira walifunga barabara
kwa magogo wakidai kuwa wamechoshwa na
ajali katika eneo hilo na kuitaka serikali kupitia
wakala wa barabara nchini Tanroads kuweka
matuta ili kupunguza ajali.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post