Wananchi Babati wamzuia mkandarasi wa umeme REA kupitisha kwenye maeneo yao.

Wananchi wa kaya zaidi ya 80 katika kitongoji
cha Mkanyageni mjini Babati mkoani Manyara
wamemzuia mkandarasi anaejenga mradi wa
usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na
wakala wa nishati vijijini (REA) kwa kufukia
mashimo ya nguzo za msongo wa umeme huo
wakipinga kupitisha nguzo kwenye viwanja vya
makazi na mashamba yao bila ya makubaliano
kwa lengo la kuelekeza mradi huo kwenye shule
binafsi badala ya kuelekeza kwenye makazi yao.
Wakilalamikia mradi huo mbele ya mwenyekiti wa
serikali ya mtaa huo wa sawe na kumtuhumu
kuwa chanzo cha mgogoro huku wakidai
ameshiriki kumuongoza mkandarasi wa kampuni
ya china iliyopewa zabuni hiyo kubadili mchoro
wa ramani na kukwepa makazi yao pasipo
ushirikishwaji wa wananchi ili kuinufaisha shule
ya kutwa kupatiwa umeme wa gharama ya
shilingi 27,000/= badala ya wakazi hao ambao ni
wengi watalazimika kulipia umeme wa Tanesco
wenye gharama ya shilingi zaidi ya shilingi
320,000/=.
Nae, meneja wa shirika la ugavi la umeme
(Tanesco) mkoani Manyara Bw Gerson Manase
amekiri kuwepo kwa mgogoro huo
uliomsababishia mkandarasi kusimamisha zabuni
hiyo kwa kufukia mashimo na kuahidi kwamba ili
kuondoa mgogoro huo Tanesco kupitia bajeti
yake ya 2016 imejumuisha kitongoji hicho
kupatiwa umeme.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Babati Bw Cripin
Meela ameingilia kati mgogoro huo kwa kukutana
na uongozi wa Tanesco pamoja na mtaa na
kukubaliana shirika hilo kuongeza nguzo 27 na
kuwapatia umeme wa Tanesco badala ya mradi
wa REA utakaonufaisha wateja wachache huku
akikeme wanasiasa kuacha kuwa chanzo na
wananchi kuacha kumzuia mkandarasi.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post