Wafanyabiashara 4 wakiwemo 3 raia wa Kenya wamekamata kwa uharibifu wa misitu Tanga.

Wafanyabishara wanne wakiwemo watatu raia wa
Kenya wametiwa mbaroni na jeshi la polisi baada
ya kukutwa na shehena ya magunia ya mkaa, na
nguzo ambazo miti yake imevunwa kinyume cha
sheria katika misitu ya hifadhi wilayani Mkinga
kwa ajili ya kusafirishwa falme za kiarabu kupitia
bandari ya Mombasa.
Hatua hiyo inafuatia operesheni maalum
iliyofanywa kwa pamoja na jeshi la wananchi
(JWTZ), jeshi la polisi na askari wa hifadhi ya
taifa (TANAPA) kufuatia raia wema kusaidia
kutoa taarifa kuwa umebainika kuwepo kwa
mtandao mkubwa wa kuvuna misitu ya hifadhi
kisha kusafirisha bidhaa zake katika falme za
kiarabu kupitia nchini Kenya.
Akifafanua kuhusu operesheni hiyo, meneja wa
misitu wilayani Mkinga Bwana Frank Chambo
amesema kundi la mtandao huo unaojihusisha na
uvunaji wa nyara za serikali kutoka nchini Kenya
linalodaiwa kuwa na watu zaidi ya 200 katika
msitu wa hifadhi wa Mwakijembe ni kubwa hivyo
inahitajika nguvu ya ziada kuweza kukabiliana na
kundi hilo ambalo linakiuka makubaliano baina ya
nchi hizo mbili ya kuheshimu raslimali za
mwenzake.
Hata hivyo mmoja kati ya viongozi wanaongoza
mtandao huo nchini Kenya aliyefika wilayani
Mkinga kwa ajili kujua mustakabali wa wenzao
kutiwa mbaroni, Tito Mayui amesema wamekuwa
wakiwatumia baadhi ya viongozi wa serikali ngazi
za vijiji na kata kwa kuwalipa fedha wakati
wanapopitisha shehena za mkaa na vigogo
wakidai kuwa walidhani kuwa fedha hizo
wanazifikisha katika mamlaka husika lakini
kumbe zinaishia mikononi mwao.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post