Viongozi wadini ya kikiristo na kiislamu mkoani
Morogoro wameungana kuunda kamati itakayo
shirikiana na serikali ya wilaya ya Mvomero
kumaliza tatizo la migogoro ya wakulima na
wafugaji ambayo imekuwa ikisababisha mauaji ya
watu na uharibifu wa mali huku wengine wakibaki
na vilema vya kudumu.
Wakizunguza katika kikao kilichoitishwa na
jumuiya ya kikirito Tanzania (CCT) viongozi hao
wa dini akiwemo askofu wa kanisa la KKKT jimbo
la Morogoro Ole Mameo wameiomba serikali
kushirikiana na kamati waliounda ilikuhakikisha
wanafanya kazi pamoja na kumaliza migogoro
ambayo imekuwa ya mara kwa mara inayo
gharimu maisha ya watu.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mvomero
Bi, Betty Mkwasa amewapongeza viongozi hao
nakuahidi kutoa ushirikiano wa dhati juu ya
mikakati ya kumaliza migogoro ya ardhi ambapo
amewataka kamati iliyoundwa kufika ofisini
kwake nakuanza kupanga mikakati ya kuanza
zoezi hilo huku mkurugenzi wa jumuiya za
kikiristo Tanzania John Mapesa akieleza uundaji
wa kamati hizo nikwakila wilaya ambazo zina
migogoro ya kila aina.
Uncategories
Viongozi wadini ya kikiristo na kiislamu
mkoani Morogoro wameungana kuunda kamati
itakayo shirikiana na serikali ya wilaya ya
Mvomero
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon