UWEZO WAKO
NI ZAIDI YA VYETI
ULIVYONANVYO
Kuna watu wanajidharau sababu kwenye vyeti vyao havipo vizuri. Lakini kuna watu wanalinganisha uwezo wao na vyeti vyao sababu vyeti vipo vizuri. Wote kwa pamoja nawaambia uwezo wenu upo zaidi ya hayo makaratasi au tuviite vyeti kwa kuvipa heshima. Uwezo wako ni mkubwa mnoo kiasi kwamba hakuna mtu anayeweza kuupima uwezo huo isipokuwa aliyekuumba tu.
Ukiamini akili yako mwisho wake ni kwenye alama ulizopata darasani hata kama umepata 100% bado unakuwa hujaelimika. Na hata kama uliwahi pata alama hadi 0% kama ndipo hapo unaamini uwezo wako umeishia basi utaendelea kupata sifuri katika mambo mengi sio shuleni tu. Mimi naamini uwezo wako ni mkubwa sana lakini hujagundua tu kama unauwezo zaidi ya hapo.
Nani alikufundisha kuongea na ukasema ma..ma au baaaba. Nani alikuingia ubongoni kwamba uanze kutembea baada ya kusimama dede. Uliimbiwa tu kasimama peke yake kamuona mchumba wake. Alafu ukaanza kutembea. Kumbe unahitaji mtu mmoja tu kukuimbia kuwa unaweza kufanya makubwa. Hata ulipodondoka bado ulisimama ukanyanyua mguu. Simama na leo onyesha uwezo wako ni zaidi ya vyeti. Kwenye vyeti wamekupima wengine tena wakati mwengine kwa kukariri vitu ambavyo hujawahi wala hutakuja vifanyia kazi. Leo jipime mwenyewe ujione jinsi ulivyo na uwezo zaidi ya vyeti na alama unazopata.
Ukijidharau sababu ya alama au cheti au ukijivuna sababu ya alama au cheti. Tena hujawahi fanyia kazi unayojivunia au kujidharau kwayo. Ujue hukuenda shule kujifunza hivyo ulienda shule kujiharibu zaidi. Shule ni kama karakana ya kufanyia majaribio na sio kusoma maandishi na kuyaacha katika vyeti.
Tunakoelekea vyeti vinakuwa kama kitambulisho cha kukutambulisha ulipitaga eneo moja linaitwa shule. Na sio kuaminika sababu tu unavyeti. Sababu hata waajili washatambua uwezo wako unatakiwa uwe zaidi ya vyeti.
Sio kwamba navidharau vyeti hapana, lakini kama umeenda shule ili upate cheti tu basi kwako uwezo wako utakuwa chini ya cheti. Lakini kama umeenda shule kwa ajili ya kupata elimu basi utapata viwili cheti na elimu. La sivyo utakuwa umeenda shule kununua cheti na ndio sababu wengi hatuwezi kuyatumia tuliyoyasoma kutufanya kuwa wagunduzi au wafumbuzi wa matatizo. Kama kuna watu wamefanya makubwa na hawana vyeti basi ujue unaakili na uwezo mkubwa zaidi ya alama na vyeti.
EmoticonEmoticon