Picha ya maktaba ikimwonyesha
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(Maelezo), Assah Mwambene akiwa
ameshika gazeti la Mawio Aprili 22,
2014 alipokutana na wanahabari
baada ya gazeti hilo kuandika habari
kuhusu hati ya Muungano.
Kwa ufupi
Kamanda amesema wanatakiwa
kutoa maelezo juu ya habari
ambazo wamekuwa wakiandika
Habari
SUNDAY, JANUARY 17, 2016
Polisi
yawasaka
wahariri
Mawio
Picha ya maktaba ikimwonyesha
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(Maelezo), Assah Mwambene akiwa
ameshika gazeti la Mawio Aprili 22,
2014 alipokutana na wanahabari
baada ya gazeti hilo kuandika habari
kuhusu hati ya Muungano.
By Kalunde Jamal, Mwananchi
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam
linawasaka wahariri na mmiliki wa
gazeti la Mawio kutokana na habari
mbalimbali ambazo wamekuwa
wakichapisha.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu
ya Dar es Salaam, Simon Siro alisema
jana kuwa wahariri hao wanatafutwa
kwa ajili ya kusaidia uchunguzi
unaofanyika kuhusu habari
walizokuwa wakiziandika.
Sirro alisema wamekuwa wakiandika
na kuchapisha habari ambazo zina
utata, hivyo wanatafutwa kwa ajili
ya kuthibitisha ukweli wake.alisema
Siro.
Mbali na kusakwa kwa wahariri hao,
jana kwenye mitandao ya kijamii,
ilisambaa taarifa iliyoonekana kama
tangazo la Serikali ya kulifungia
maisha gazeti hilo bila kueleza
sababu za hatua hiyo, ingawa
halikuwa na saini ya Waziri wa
Habari, Nape Nnauye aliyetajwa
kuandaa tangazo hilo.Nape
alipotafutwa na Mwananchi kwa
simu kuzungumzia suala hilo, alijibu
kwa ujumbe mfupi, “samahani, nipo
kikaoni tuma msg!” Hata
alipotumiwa ujumbe huo hakujibu.
Hakuna kiongozi yeyote wa Serikali
aliyepatikana jana kuzunguzia
taarifa hiyo.
Hata hivyo, baadaye usiku, Idara ya
Habari (Maelezo), ilitoa taarifa kuwa
Waziri Nape atazungumza na
waandishi wa habari leo saa sita
mchana, lakini haikueleza katika
mkutano huo utakaofanyika katika
ukumbi wa idara hiyo atazungumzia
nini.
Kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti
ya mwaka 1976, Waziri wa Habari
anaweza kulifungia gazeti wakati
wowote akijiridhisha kwamba
halikuendana na masilahi ya umma.
Sheria hiyo imekuwa ikipingwa kwa
maelezo kuwa imepitwa na wakati
na inakandamiza uhuru wa habari
EmoticonEmoticon