SABABU ZA KUJIUZURU KATIBU MKUU WA YANGA

Habari kubwa kwa sasa katika soka la bongo ni kuhusu aliyekuwa katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiborohakutangaza kujiuzulu nafasi yake, wengi walikuwa wanaripoti kuwa katibu mkuu huyo katangaza kujiuzulu kwa shinikizo na sio maamuzi yake, kitendo ambacho kilifanya mchana wa January 23 wapenzi na wanachama wa klabu hiyo wakusanyike makao makuu na kupinga uamuzi huyo katikavyombo vya habari.

Kwa upande wa Dk Jonas Benedict Tiboroha ameeleza sababu ya kujiuzulu ni yeye mwenyewe kaamua wala sio shinikizo, sababu kubwa iliyomfanyaTiboroha ajiuzulu ni kuongezewa majukumu ya uhadhiri wa chuo kikuuDar Es Salaam, kitu ambacho kimemfanya aachane na nafasi yake hiyo Yanga.

Ukweli nimejiuzulu kwa makubaliano tu kwa sasa nipo busy na kazi zangu, kiukweli watu wanapaswa kujua kuwa mimi ni mhadhiri na shughuli zangu, mwenzetu mmoja atakuwa hayupo, kwa hiyo nimeongezea majukumu na muajiri wangu ambao ni chuo kikuu DSM, hivyo siwezi kumudu kuendelea kuongoza Yanga” >>> Tiboroha

Previous
Next Post »

Ads Inside Post