Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Mh.
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
amemuongezea muda wa utumishi kwa mwaka
mmoja Mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini
Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange ambaye
muda wake wa utumishi ulikuwa unamalizika
kesho.
Akiongea na vyombo vya habari leo jijini Dar es
salaam Makao makuu ya jeshi hilo, Generali
Mwamunyange alitoa taarifa ya uteuzi wa Rais
kwa maafisa wanane waandamizi wa jeshi hilo
ikiwa ni pamoja na mnadhimu mkuu mpya wa
jeshi Luteni Jenerali Venance Mabeyo.
Uteuzi wa nafasi hizo kwa maafisa wandamizi wa
jeshi hilo kunafuatia kustaafu kwa maafisa
waandamizi ambao muda wao wa utumishi
katika jeshi hilo unamalizika kesho tarehe 31
January 2016.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon