MKATAJI vichwa vya raia kutoka mataifa ya
magharibi katika kundi la kigaidi la Dola ya
Kiislam (IS), Mohammed Emwazi,
ametangazwa kuuawa.
Emwazi anatambuliwa zaidi kwa jina la
Jihadi John, ndiye aliyekuwa akitumiwa zaidi
kwenye video ambazo zilikuwa zikioneshwa
na kundi hilo wakati wa kutekeleza mauaji ya
raia wa mataifa ya magharibi walilokuwa
wakikamatwa na kundi hilo.
Raia huyo wa Uingereza alikuwa akitafutwa
kwa udi na uvumba na wanajeshi wa mataifa
ya magharibi kutokana na kuhusika zaidi
katika kutesa na kuua raia wa mataifa hayo
walikokamatwa na kundi hilo.
IS wametangaza kifo cha Emwazi katika
jarida lao la mtandaoni lijulikanalo kwa jina la
Dabiq. Taarifa ya IS inaeleza kuwa
mwanamgambo huyo aliuawa kwenye
shambulio lililotekelezwa na ndege
zisizokuwa na rubani Novemba mwaka jana.
Hata hivyo, Marekani baada ya kufanya
shambulio lake dhidi ya Emwazi mwaka jana
mjini Raqqa, ilieleza kutokuwa na uhakika wa
kumuua mwanamgambo huyo.
Emwazi alionekana mara kwa mara kwenye
video za kikatili za kundi hilo, miongoni
mwayo ni ile iliyoonesha akiwakata shingo
mateka kutoka mataifa ya magharibi
wakiwemo Muingereza David Haines ambaye
alikuwa mfanyakazi wa shirika la kutoa
misaada na Alan Henning ambaye alikuwa
dereva wa teksi.
Lakini IS kwenye tangazo lao walimtaja
Emwazi kwa jina la Abu Muharib al-Muhajir
kutokana na kupenda kulitumia ndani ya
kundi hilo wakati wa uhai wake.
IS wanaeleza kuwa Emwazi alifariki dunia
Novemba 12 kwenye gari lililoshambuliwa na
ndege zisizo na rubani katika mji wa Raqqa.
Waliweka picha ya Emwazi akionekana
kutabasamu. Alizaliwa Kuwait mwaka 1988
na kuhamia Uingereza mwaka 1994.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon