MH MWIGULU NCHEMBA AKITUMBUA VIJIPU UCHUNGU HUKO TUNDURU, RUVUMA.

Ufuatiliaji wa Ugawaji wa pembejeo kwa
wakulima,Nimefika wilaya ya Tunduru,Kata
ya Nandembo na kata jirani kwaajili ya
kujiridhisha na namna ugawaji wa pembejeo
unavyofanyika kwa wakulima.
Nimekutana na mchezo mchafu wa ugawaji
wa pembejeo unaohusisha wakala wa
pembejeo kula njama na viongozi wa serikali
wa kata na vijiji kuwasainisha wakulima
kuwa wamepokea pembejeo(Mbegu
+Mbolea) ilia hali pembejeo hizo zinaishia
mifukoni mwa wakala.
Baadhi ya wakulima ambao sio waaminifu
wanadiriki kupokea fedha kidogo
iliwamuachie wakala zile pembejo akauze
sehemu nyingine kwa bei ya juu ili hali ni
ruzuku iliyotolewa na serikali kwaajili ya
kuwasaidia wakulima kuboresha kilimo chao.
Kwa hatua za awali kwa ubadhilifu
uliofanywa na Uongozi wa kata ya
Nandembo na mawakala waliopewa dhamana
kusambaza pembejeo hizo wote
wamekamatwa na jumatatu kupitia Kamati
ya Ulinzi ya wilaya watapandishwa
kizimbani.
Lakini kuanzia sasa wakala Bw.Zuberi
Namahala na Bw.Ibrahim Mohamed Ibrahim
mbali ya kukamatwa na kufikishwa
mahakamani,kuanzia sasa wamefutwa
kwenye orodha ya mawakala wa pembejo.
Natoa rai kwa Viongozi,Mawakala wa
pembejeo na wakulima wote popote walipo
kuhakikisha lengo la serikali la kuinua sekta
ya Kilimo inafanyika kwa uaminifu na
ufanisi,kwa yeyote yule anayeshiriki
kuhujumu na kujinufaisha kupitia pembejeo
zinazotolewa na serikali hatakwepa mkono
wa serikali.
Imetolewa na Mwigulu L. Nchemba,
Waziri wa Kilimo,ufugaji na uvuvi.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post