Bulaya amtaka Wasira kortini

Bulaya alikuwa akiwasilisha hoja
za pingamizi aliloweka dhidi ya
shauri la madai namba moja la
mwaka 2015 lililofunguliwa
mahakamani hapo na Magambo
Masato na wenzake watatu
wakiiomba mahakama kutengua
matokeo yaliyompa ushindi
mbunge huyo aliyekuwa kada wa
CCM kabla ya kuhamia Chadema. Mwanza. Mbunge wa Bunda Mjini
(Chadema), Ester Bulaya amemtaka
aliyekuwa mpinzani wake katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana,
Stephen Wasira (CCM) kuacha
kujificha nyuma ya wapigakura,
badala yake ajitokeze kortini
kupinga ushindi wake.
Kupitia kwa wakili wake, Tundu
Lissu, mbunge huyo alidai mbele ya
Jaji Ramadhan Mohamed wa
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza
kuwa, ingawa jina la Wasira halimo
kwenye orodha ya wadai, lakini
ametajwa kwenye hoja zote za
walalamikaji ambao pia wamekiri
kwa hati ya kiapo kuwa hoja
walizowasilisha mahakamani
walizipata kutoka kwake.
Bulaya alikuwa akiwasilisha hoja za
pingamizi aliloweka dhidi ya shauri
la madai namba moja la mwaka 2015
lililofunguliwa mahakamani hapo na
Magambo Masato na wenzake watatu
wakiiomba mahakama kutengua
matokeo yaliyompa ushindi mbunge
huyo aliyekuwa kada wa CCM kabla
ya kuhamia Chadema.
“Kwa nini Wasira asijitokeze
mwenyewe kuja mahakamani kudai
haki yake iliyokiukwa badala ya
kujificha nyuma ya wapigakura
ambao kimsingi walipata haki yao ya
kikatiba ya kupiga kura?” alihoji
Lissu.
Wakili huyo alidai maelezo yote
kwenye hati ya madai ya
walalamikaji hayataji haki yoyote ya
mpigakura iliyokiukwa, bali
anayedaiwa kunyimwa haki ni
Wasira ambaye siyo mmoja wa
walalamikaji.
Bulaya anaiomba mahakama hiyo
kutupilia mbali maombi hayo akidai
walalamikaji hawana haki kisheria
kupinga matokeo ya uchaguzi.
Miongoni mwa madai ya msingi ya
walalamikaji wanaowakilishwa na
mawakili Constantine Mutalemwa na
Denis Kahangwa, wanadai Wasira
alikataliwa ombi la kuhesabu wala
kuhakiki kura.
Walalamikiwa wengine ni
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la
Bunda Mjini. Uamuzi wa pingamizi
hilo utatolewa Januari 25.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post