Mahakama yafuta kesi ya Tundu Lissu.
Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, jana ilifuta
kesi ya kupinga matokeo ya ubunge yaliyompa
ushindi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu
(Chadema) katika uchaguzi mkuu wa mwaka
jana.
Mdai katika kesi hiyo, ambaye pia alikuwa
mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Jonathan
Njau, aliamua kuiondoa kesi hiyo kwa madai
kuwa inampotezea muda wa kufanya shughuli
zingine ikiwa ni pamoja na kushindwa kulipa
gharama za kuendesha kesi, Sh. milioni 15.
Katika shauri hilo Njau alikuwa akilalamikia
utaratibu uliotumika katika kuhesabu kura
zilizompa ushindi Lissu, hivyo akataka kura hizo
zirudiwe kuhesabiwa upya, jambo lililopingwa na
mhusika.
Mbele ya Jaji Barker Sahel, Wakili wa Njau,
Geofrey Wasonga, alisema mteja wake ameamua
kuifuta kesi hiyo ili kumpa nafasi ya kufanya
majukumu mengine pamoja na kumpa uhuru
Lissu wa kutekeleza majukumu yake ya kibunge.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya
mahakama, Lissu alisema alikuwa na uhakika wa
kushinda kesi hiyo kwa kuwa ilikuwa na makosa
mengi ya kisheria yanayolingana na ile ya kipindi
kilichopita.
Lissu alisema kabla ya kufutwa kwa shauri hilo,
mdai alishawasilisha mara mbili maombi ya
kutaka kupunguziwa gaharama za kesi na
imepita zaidi ya miezi miwili ameshindwa kulipa.
Alisema latika kesi hiyo aliweka mapingamizi sita
na hata kama angelipa gharama hizo asingeweza
kuyavuka kwa kuwa kesi hiyo ilifunguliwa kwa
ushabiki wa kisiasa.
Wakili aliyekuwa akisaidiana na Lissu, Fred
Kalonga alisema walijiandaa kikamilifu katika kesi
hiyo na kwamba wangeshinda mapema kuliko
ilivyokuwa mwaka 2010, katika kesi iliyofunguliwa
na wananchama watatu wa CCM.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon