KAMANDA SIRRO AAMUA

Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya
Dar es Salaam Simon Sirro ameeleza kuanza
kutumia mikutano na wananchi sambamba na
mawasiliano ya simu za viganjani kama hatua ya
kukomesha uhalifu, magendo biashara haramu
sambamba na kubaini askri wake wanaofanya
kazi kinyume cha sheria.
Katika hatua hiyo ambayo pia alitembelea kituo
kilichochomwa moto na wananchi mwaka jana
kwa nia ya kuanza ukarabati kamanda Sirro
amewaeeleza wananchi wa Bunju nia ya
mikutano yake ikiwa ni kuwa karibu na wananchi
ambao wanao uwezo wa kulisaidia jeshi hilo
kubani uharifu ikiwemo uuzaji bangi na pombe
haramu ya gongo.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post