MAFURIKO DODOMA

Zaidi ya wakazi 400 wa kijiji cha
Mpunguzi kilichopo manispaa ya Dodoma hawana
mahala pa kuishi baada ya nyumba 70 kusombwa
na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa
iliyonyesha katika eneo hilo usiku wa kuamka leo.
Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya wakazi
waliokumbwa na mafuriko hayo wamesema hali
hiyo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kwa kile
nachodai ni udogo wa daraja lililopo barabara kuu
ya Dodoma Iringa linalokatisha eneo hilo
kushindwa kuhimili wingi wa maji na kujenga
mkondo ambao umesambaa na kuyafikia makazi
yao na kuzua balaa hilo.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post