Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania mzunguko
wa kumi na nne unatarajiwa kuendelea
wikiendi hii kwa michezo nane kuchezwa.
Katika uwanja wa Karume jijini Dar es
salaam, Maafande wa JKT Ruvu
watawakaribisha Maafande wa Mgambo
Shooting,
Toto Africans watakua wenyeji wa Tanzania
Prisosns uwanja wa CCM Kirumba, huku
Stand United wakicheza dhidi ya Kagera
Sugar uwanja wa Kamabarage mjini
Shinyanga.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Simba
SC watawakaribisha wakata miwa wa
Mtibwa Sugar ,Mbeya City watakipiga na
Mwadui FC uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Huko Tanga Coastal Union watawalika
Majimaji mchezo utaopigwa katika dimba la
Mkwakwani, huku Azam FC wao watapima
ubavu na African Sports mchezo ukianza
saa 1 usiku.
ligi hiyo itaendelea tena siku ya Jumapili
kwa mchezo mmoja uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam, ambapo Young African
watawakaribisha Ndanda FC kutoka
Mtwara.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon