Jeshi la Polisi mkoani Arusha limemkamata na kumfikisha mahakamani chini ya ulinzi mkali askari, polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU

Jeshi la Polisi mkoani Arusha
limemkamata na kumfikisha mahakamani chini ya
ulinzi mkali askari, polisi wa kikosi cha kutuliza
ghasia FFU Rafaeli Paulo kwa tuhuma za
kumbaka mwanafunzi mwenye wa kidato cha sita
wenye umri wa miaka kumi na sita.
Akisoma shitaka namba 13 ya mwaka 2016
hakimu wa mahakama ya wilaya ya Arusha
Jasmini Abduli amesema mnamo tarehe 16
mwezi Januari mwaka huu 2016 mtuhumiwa
Rafaeli Paulo mwenye umri wa miaka 25
alimbaka mwanafunzi wa kidato cha sita mwenye
umi wa miaka 16 ambalo ni kosa kinyume na
kifungu cha 130 kifungu kidogo cha kwanza na
cha pili na kifungu cha 131cha makosa ya jinai
sura ya 16.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post