Baada ya kutolewa Mapinduzi Cup, Simba yafanikiwa kulipiza kisasi kwa Mtibwa Sugar Namatokeo mengine

Baada ya wekundu wa msimbazi Simba
kutolewa katika hatua ya nusu fainali ya
michuano ya Kombe la Mapinduzi na Mtibwa
Sugar ya Manungu Morogoro . January 16 katika
mchezo wa Ligi Kuu walikutana tena, hiyo
ilikuwa ni nafasi kwa Simba kulipa kisasi kwa
Mtibwa Sugar au kuendeleza rekodi ya kupokea
vipigo.
Simba ambayo ilikuwa inacheza mchezo wake
wa kwanza wa Ligi Kuu toka ianze kufundishwa
na kocha wake msaidizi Jackson Mayanja,
ambaye kwa sasa anasimama kama kocha mkuu
baada ya Simba kumfukuza kocha wake wa
kiingereza Dylan Kerr siku kadhaa nyuma, Simba
kupitia kwa mshambuliaji wake wa kimataifa wa
Uganda Hamisi Kiiza, walifanikiwa kuibuka na
ushindi wa goli 1-0.
Goli la Simba lilifungwa na Hamisi Kiiza dakika
ya 8 kipindi cha kwanza, goli hilo lilionekana
kuwagawanya Mtibwa Sugar kwa kipindi cha
kwanza, kwani Simba kwa kiasi kikubwa
waliutawala mchezo, Mtibwa walijaribu kutafuta
goli la kusawazisha kwa bidii kipindi cha pili,
jitihada ambazo hazikuzaa matunda.

Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa January
16
JKT Ruvu 1 – 5 Mgambo JKT
Toto Africans 0-1 Tanzania Prisons
Stand United 1-0 Kagera Sugar
Mbeya City 1-0 Mwadui FC
Coastal Union 1-1 Maji Maji FC

Previous
Next Post »

Ads Inside Post