ANGALIA TV KUPITIA COMPUTER YAKO AU SIMU YAKO SEHEMU 1

SEHEMU 1: Tumezoea katika maisha yetu tukiangalia Tv basi
huduma ile tunaipata kupitia madishi, cable au
antenna. siku zinavyosogea mbele na technology
ndivyo inavyokuwa na ndio jinsi madish na
antenna vinavyopitwa wakati. leo kwenye uzi huu
tutaangalia IPTV.
Ni nini hii IPTV?
IPTV ni kifupi cha Internet Protocal TeleVision.
Hii ni aina ya uangaliaji TV kupitia mtandao wa
internet ambapo kituo cha TV badala ya kutumia
satelite dish au cable wenyewe wanarusha
matangazo kwa internet.
Unawezaje kuangalia IPTV?
Utahitaji kifaa chenye internet na uwezo wa
kustream ili kuweza kuangalia kama vile
smartphone, tablet, laptop, desktop hadi TV
zenye internet zinaweza kustream.
Internet yenye speed gani inahitajika?
Internet yoyote hata ya edge inaweza kustream
ila iwe na latency nzuri, zipo stream zinahitaji
speed ya 200kbps tu (25KBps). Kama una
latency ndogo hata internet iwe na speed vipi
huwezi kustream live utastream tu vitu ambavyo
si live
Je software gani inatumika kustream hizo TV?
Kikawaida browser yenye flash au html5 inaweza
kustream tv lakini ukitaka kustream vizuri zaidi
software kama VLC au KODI ni muhimu.
Kutokana na uhaba wa links za VLC
nitazungumzia zaidi jinsi ya kutumuia KODI
kuangalizia IPTV.
KODI ni nini?
KODI ni software (media centre) ambayo
hutumika kuubadili muonekano wako wa simu
uwe kama TV na kuweza kuenjoy TV unazotumia
na inapatikana kwenye simu, tablet, computer
hadi TV.
Kuidownload nenda website yao hii hapa chini, ni
bure haiuzwi
Downloads | Kodi
Nikishadownload kodi nini kinafuatia?
Utahitaji ku install plugin ili uweze kuangalia TV
online. Click video add on halafu chagua
watchmojo, install halafu ifungue tuone kama
itafanya kazi.
KODI imefanya kazi, je siwezi angalia mpira na
vipindi vyengine?
Unaweza angalia mpira chanel unayotaka
kuanzia za ki-Africa kama Super sport, za Ulaya
kama Sky sport, za Asia kama Bein sport hadi za
kimarekani kama NBC cha muhimu uwe na plugin
(add ons) husika, hizi plugin za mpira na michezo
mengine zinapatikana tu internet mfano mimi
plugin yangu ninayotumia inaitwa Vdtube25 ina
channel nyingi sana kuanzia mpira hadi movie.
Hio hapo juu sky sport 3
Uzuri wa hizi plugin za kodi zipo TV ni HD na
nyengine ni full HD kabisa hivyo internet yako tu.
Malipo?
Kila kitu kuanzia juu hadi hapa ulipofikia ni bure
hutoi pesa, ila hizi plugin za bure haziaminiki
zipo za kulipia ambazo hazikati ovyo. Mimi
sijawahi kulipa natumia tu bure

Previous
Next Post »

Ads Inside Post