Inaweza kutokea unasafiri kwenye gari hivi labda toka Dar mpaka kahama au Dar mpaka Mwanza kwenye basi la abiria pekeyako, unaweza kujifariji kwa kuchekicheki nje mazingira, ukachezea simu yako au ukaendelea zako na safari kwa kusikiliza muziki au kuangalia TV kwenye basi, kwenye ndege je inakuwaje?
Jamaa mmoja Alex Simon mtalii kutokaAustria, alijikuta kwenye level za kistaa hivi au mtu fulani VIP kwenye ubora wake baada ya kujikuta akiwa ndio abiria pekeake ndani ya ndege ya abiria zaidi ya 100… alitoka zake Manilakwenda Boracay ndani ya Ufilipino kwa ajili ya kutalii tu !!
Baada ya Simon kuingia kwenye ndege alianza kupiga stori na marubani baadae akaungana na wahudumu wawili wa ndege wakiendelea na stori mpaka alipotua
Video ya jamaa mwenyewe hii hapa mwanzo mpaka mwisho wa safari
EmoticonEmoticon