Fahamu jinsi ya kutuma GIF’s kwenye WhatsApp

WhatsApp wanazidi kufurahisha watumia wa WhatsApp kwani sasa watumiaji wa iPhone wanaweza kutuma GIF’s kupitia WhatsApp.

Katika miaka kadhaa tulizoea kuona mtu akikutumia GIF’s kwenye Facebook, iMessage (wanaotumia iPhone) na hata kwenye Twitter lakini na WhatsApp wameleta huduma hiyo ingawa kwa sasa inapatikana kwa wale wanaotumia simu janja za iPhone au kwenye programu endeshaji ya iOS.
GIF ni nini?
GIF (Graphics Interchange Format) ni picha ambayo inaigiza tendo fulani pasipo kusikia kwa sauti yoyote kwa muda mfupi sana. Kwenye iOS ni GIF’s yenye urefu usiozidi sekunde sita tu ndio unaweza kumtumia mtu.
GIF ya Oprah akishangilia jambo fulani.
Namna ya kutuma video kama GIF.
Si rahisi sana kutuma video za GIF kwenye iOS na hasa kama si mpenzi wa kutaka kujua zaidi lakini pia si vigumu sana kuweza kujua jinsi ya kutuma video kama GIF. Cha kuzingatia ni kwamba GIF unayotaka kuituma isizidi urefu wa sekunde 6 .
1. Chagua video unayotaka kuituma kama GIF kutoka kwenye orodha ya video ulizonazo kwenye simu yako (kwa sasa ni kwa watumiaji wa iPhone tu!).
2. Baada ya kuchagua video unayotaka kuituma kama GIF, upande wa kulia juu utaweza kuchagua kuituma kama ilivyo (video) au kama GIF-chagua ‘GIF’ kuweza kuifanyia marekebisho video hiyo ili iwe katika urefu usiozidi sekunde sita.

Namna ya kutuma picha kama GIF.
Picha nayo unaweza kuituma kama GIF na si tofauti sana kama jinsi ya kutuma video kama GIF, ni unachagua picha unayotaka kuituma kama GIF kisha inaigusa mguso wa 3D (3D Touch) kisha itatokea menu na utachagua ‘Send as GIF ‘.

Je, GIF inapatikana watumiaji wa Android/WhatsApp Web?
Kwa sasa maboresho hayo yanapatikana kwenye iOS tu ila hivi karibuni maboresho hayo yataweza kupatikana katika WhatsApp Android. Hata hivyo, wanaotumia WhatsApp Beta wataweza kutumia GIF. WhatsApp Web inaweza kusoma kitu kilichotumwa katika mfumo wa GIF ila si kutuma.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post