MAMBO MATANO MUHIMU KUHUSU GB WHATSAPP
Posted by ITPhidel on NOVEMBER 9, 2016
GbWhatsapp ni whatsapp ambayo imeongezewa mambo mengi ambayo hayapo kwenye whatsapp tuliyoizoea. Kwa kizungu tunaweza tukaita custom whatsapp. Gbwhatsapp ina mambo mengi ya muhimu ambayo huwezi kuyakuta kwenye whatsapp ya kawaida. Leo nitazungumzia mambo matano ya muhumi yaliyopo kwenye Gbwhatsapp lakin hayapo kwenye whatsapp.
Bila kupoteza muda, Gbwhatsapp inakupa uwezo wa kubadili launcher icon ya whatsapp na kuipa muonekano unaotaka wewe. Mfano tazama picha chini na utagundua whatsapp yangu ya kawaida ina icon ileile ambayo kila mtu anayo lakin kwa vile nina Gbwhatsapp nimeweza kubadilisha icon yangu na kuifanya kuwa nyekundu
Kitu kingine muhimu kuhusu GBwhatsapp ni lock chat.Lock Chat inakuwezesha kulock chat ya mtu mmoja hata mtu akijaribu kubonyeza chat ya huyo mtu basi whatsapp itamwambia aweke password ili aweze kusoma hiyo chat. Hii ni nzuri kwa wale mademu zetu wa kibongo wanaopenda kubonyeza chat za wanawake wengine ili kujua unachat nini.. mfano tazama picha chini nimefungua chat ya phonetrick halafu naenda kwenye setting kisha na bonyeza kipengele cha chat lock kisha whatsapp itakwambia uweke password.
Jambo lingine zuri kuhusu GBwhatsapp ni uwezo wa ku-copy status ya mtu. Wengi tunajua kwamba kwenye whatsapp huwezi ku copy status mpaka uandike sehemu halafu ndio ukaweke kwako lakin kwenye Gbwhatsapp mambo kama hayo yanawezekana na ni rahisi kama kunywa maji vile. Ukitaka ku-copy status ya mtu unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye status ya huyo mtu unayotaka ku-copy kisha bonyeza na kushikilia utaona ujumbe unaosemastatus copied to clipboard kama inavyo onekanan kwenye picha chini
GbWhatsapp ina kuwezesha kuchat kwenye magroup kijanja zaidi kushinda ilivyo kwenye Whatsapp ya kawaida. Mfano kwenye Gbwhatsapp ukiwa kwenye group na unataka ujumbe wako utume kwa mtu flani basi unachotakiwa kufanya ni kuandika alama @ kisha utaona majina ya watu ambao waliopo kweye group na utabonyeza jina unalotaka kama inavyo onekana kwenye picha chini
GBwhatsapp inakuja na themes ambazo zinakupa muonekano mzuri kushinda ilivyo kwenye whatsapp kawaida. Themes imeifanya Gbwhatsapp kuwa nzuri zaidi ya whatsapp ya kawaida. Endapo utataka kubadilisha theme kwenye Gbwhatsapp, unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye menu kisha bonyeza kipengele kinachosema Gb settings. Kwenye Gbwhatsapp unaweza kuficha blue ticks na kumfanya mtu aliyekutumia asigundue kama umesoma message zake. Pia unaweza kuzuia watu wasione last seen yako, wala wasikuone online hata kama upo online.
Kwa wale wanaotaka kujaribu Gbwhatsapp, unaweza ku-download kupitia link chini
https://linksredirect.com/?pub_id=9983CL9180&source=js&url=http%3A//www.mediafire.com/file/sh6y23kwyyye74g/GBWA3_v4.91-2.16.259_%2540atnfas_hoak.apk
EmoticonEmoticon