Njia Tano za Kulinda Data Zako Sasa

Je, wewe ni moja wa watu walio na msukumo mkubwa wa kulinda data na maisha yako ya kidijitali? Hii inakuhusu sana.
Mara nyingi tunasikia ya kwamba mitandao mbalimbali na huduma za mtandaoni zinavamiwa na wahalifu wa mitandao na katika nyakati hizo mtu wa kawaida hauna mengi unayoweza kuyafanya kukabiliana na matatizo kama hayo. Watu husema kinga ni bora kuliko kutibu yaliyojiri, hivyo kuna vitu rahisi unavyoweza kufanya kabla ya majanga ili kujilinda na uhalifu wa mitandao kama:
1. Ruhusu Roboti Kumudu Pasiwedi Yako
Kwa kawaida, akili ya binadamu haina uwezo mkubwa wa kukumbuka pasiwedi na hata kutengeneza nzuri, yenye ugumu wa kudhibiti kuvamiwa.
Mara nyingi tunatumia pasiwedi ileile kwenye tovuti mbalimbali. Hili sio jambo zuri. Linamaanisha kwamba kama mhalifu akigundua na kuvamia akaunti mojawapo unayomiliki, anaweza kuingia kwenye akaunti zako zingine.
Hili ni tatizo kubwa hasa ukizingatia watu wengi wanasemekana kufanya hivyo kwenye akaunti zao za Facebook, Google, Twitter na hata akaunti za benki za mtandaoni.
Suluhisho la jambo hili ni kutumia huduma moja ya kumudu pasiwedi zako za kompyuta na simu ambayo itaipa kila tovuti uliojisajili passiwedi isiyo na mpangilio maalumu mara kwa mara na kui-’synchronise’ kwa vitumi vyako vyote. Mifano ya huduma kama hii na ambayo inajulikana sana ni kama 1Password na LastPass.
2. Pata U2F – na Tumia Uidhinisho wa Aina Mbili
Njia nyingine ya kulinda akaunti zako ni kuhakikisha kwamba hata kama mtu ataijua passiwedi yako, hatakuwa na idhini ya kuingia kwenye akaunti hiyo moja-kwa-moja.
Ili kuingia kwenye akaunti, inabidi awe na uidhinisho wa ziada, yani tofauti na pasiwedi. Kwenye baadhi ya tovuti, hii inaweza kuwa namba ya siri inayotumwa kwenye simu yako kutoka kwa tovuti/ huduma husika (kama unavyotumiwa na WhatsApp unapo-’sign-in’), au kuanzisha app maalumu ya ziada kwenye kifaa chako ambayo itatoa namba ya siri ya kutumika mara moja.
Moja ya njia mpya kabisa kama hizi za uidhinisho wa mara mbili ni ‘U2F security key’, ambayo ni kwa kutumia kitu kinachoonekana kama flashi ya USB ya kawaida. Bila ya kifaa hicho, huwezi kuingia kwenye akaunti flani kwenye kompyuta yoyote. Kifaa kama hiki kinaweza kugharimu kama dola 15 za kimarekani (TShs 30000) ambayo ni gharama ndogo ya kukuongezea usalama wa data zako. Tayari ishaonekana kwamba ndani ya miaka michache inayokuja, makampuni makubwa yataongeza matumizi ya U2F.
3. Wezesha ‘Disk Encryption’
Kama una laptopu au simu ya mkononi ambayo haijawezeshwa na ‘Data Encryption’ na ikaipotea, ujue kwamba mtu yeyote ambae ataipata ana uwezo wa kupata data zako kirahisi.
Data Encryption ni mbinu maalumu ya kuficha data zako kwenye kifaa kwa kuzipa data hizo mfumo usiosomeka iwapo mtu akiamua kuflash hicho kifaa na kujaribu kuibua data zako. Mbinu hiyo imewekwa moja kwa moja kwenye i-phone na iPad ila kwa Windows, Android na Mac OS inabidi utumie muda wako kidogo ili kuiwezesha. Jambo hili ni la msingi kwa wale walio na ‘unyeti’ wa data zao na maisha yao ya kidijitali.
4. Weka Stika kwenye Kamera ya Kompyuta
Imejulikana kwa muda mrefu kwamba kuna watu mtandaoni wana tabia ya kuwasha kamera zilizopo kwenye laptopu zisizo za kwao kwa makusudi ya kuchungulia kila unachofanya bila wewe kujua. Hiki kitu hakitokei mara milioni kwa mwaka ila bado kinatokea ni kitu kinachotokea mara kwa mara na cha kutisha. Unaweza kujilinda na wahalifu hawa kwa kuweka stika kwenye hiyo kamera uwapo huitumii.
Unaweza kujilida na wahalifu kwa kuweka stika kwenye hiyo kamera uwapo huitumii.
5. Encrypt Mawasiliano yako ya Simu na Ujumbe
Mawasiliano ya simu na meseji ambazo makampuni ya simu yanatoa yana uwezo wa kufuatiliwa na mtu yeyote mwenye nia . Hii ina maana kwamba serikali yako au ya nchi nyingine na watu wenye maslahi ya kuiba ujumbe na mazungumzo yako kwenye simu wanaweza kupata chochote wanachotaka bila ya nguvu nyingi. Baadhi ya app za intaneti kama WhatsApp na FaceTime zinaweza kuwa nzuri ila kama ungependa usiri zaidi, fanya tafiti kidogo kupata huduma zenye usalama wa hali ya juu kama Signal inayopatikana kwenye Apple Store.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post