Tuna tumia simu zetu kufanya vitu vingi sana kucheza games, kutuma na kupokea e-mails, kununua vitu, kupiga picha, kurekodi video na hata kupiga simu (ndio bado watu wanafanya hivyo).
Sasa bila simu zetu maisha kidogo yangezidi kuwa magumu sanasana pale betri inapoishiwa chaji na simu kuzima wakati bado una matumizi na hiyo simu.
Kwa ujumla Njia ya kupunguza uishaji wa betri ni kuzima vitu vyote katika ‘smartphone’ yako ambavyo vinaifanya hiyo simu iwe ‘smart’ Lakini kwanini upitie yote hayo?
Zifuatazo Ni Njia Za Kuongeza Uhai Wa Betri La ‘Smartphone’ Yako
1. Zima
Hapana sio simu yako bali ni yale mambo yote ambayo hutumii kwa wakati huo. kwa mfano kama uliwasha ‘Bluetooth’ inabidi uizime hata WiFi , GPS services, Widgets, Location vyote vinabidi vizimwe kama havitumiki. chukua mda wako pitia ‘settings’ za simu na ufanye hayo yote
JINSI: nenda katika iOS settings au Andoid settings ili kuzima hivi vitu vyote
2. Fifisha Mwangaza
Inaweza kukushangaza kuwa kitu kikubwa kinachomaliza betri katika simu yako ni ‘screen’ kwasababu inatumia ‘power’ nyingi hapa kitu cha kufanya ni kupunguza mwangaza wa hiyo simu pia kuifanya iwe inatoa mwangaza ‘automatically’
JINSI: iOs Settings > Wallpaper & Brightness. Android Settings > Display > Brightness
3. Zima Mngurumo
Hapa ndipo watu wengi wasipojua, simu inatumia umeme mwingi inaponguruma kuliko pale inapotoa sauti. hivyo basi inabidi mingurumo yote isiyo ya lazima izimwe
JINSI: iOs Settings > Sounds. Android Settings > Sounds & Display > Phone Vibrate
4. Epuka Wallpaper Zinazobadilika badilika
Hizi Wallpaper zinaonekana nzuri pia zinavutia na kupendezesha simu laki zinamaliza betri sana kuliko wallpaper ambazo hazibadiliki hivyo inabidi ziepukwe
JINSI: iOs Settings > General > Accessibility >Reduce motion > ON. Android Settings > Sound & Display > Animation
5. Epuka simu Kufanya Automatic “App Updates’
Hii inasaidia betri kutoisha mapema tena hasa kama una app nyingi katika simu yako.Sababu usipozima simu itakua kila wakati inaangalia kama kuna update ya app yoyote kisha ifanye kuiupdate (download)
JINSI: iOs App Store > Updates . Android Google Play Store > My Apps
Kama Bado Tatizo halijapungua kuna Njia Ya Jumla Ya Kupungunza Nayo ni;
A: Kwa iOs Tuu
Watumiaji wa iphone ambao wanatumia iOs 7 wana vitu vingi ambavyo vinamaliza betri ya simu lakini pia vinaweza vikazimwa . kwanza Nenda katika Settings > General > Accessibility > turning Reduce Motion > ON hii itazuia kucheza cheza kwa mafile pale unapoyafungua . Pia Settings > General > Background App Refresh kisha uzime kila App ambayo huitumii
B: Kwa Android Tuu
Watumiaji wa Android wana njia nzuri ya kujua ni App gani inatumia Betri sana Njia ni kwenda Settings > About Phone > Battery Use ili kuona ni App gani inatumia betri sana kuliko zingine na kama ni kitu ambacho kweli hutaki kukiondoa au kukizima njia mbadala ni ku ‘download’ juice defender Hii App itafanya vitu vyote ambavyo ungefanya ili kuongeza uhai wa betri lako ‘automatically’ mfano kuzima Bluetooth na WiFi kipindi hauvihitaji.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon