Utafiti mmoja nchini Uingereza umegundua ukuaji wa utumiaji wa sigara za umeme, maarufu kimombo e-cigarettes, kumechangia kuwawezesha watu kuacha kabisa uvutaji sigara.
Utafiti huo umegundua takribani watu 18,000 nchini humo waleweza kuacha kuvuta sigara mwaka 2015 kutokana na kutumia e-cigarettes.
Utafiti huo uliofanywa na chuo cha London, (University College London) kwa kushirikiana na Shirika la Utafiti wa (Cancer Research UK) ulihusisha uangalizi wa karibu wa data za watumiaji na waachaji uvutaji sigara kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2015.
“Kwa kila watu 10,000 wanaotumia e-cigarette ili kuweza kuvuta sigara kabisa kuna wastani ya watu 580 kati ya hao watakaofanikiwa kuacha kuvuta sigara kabisa ambao wasingeweza kuacha kama e-cigarette zisingekuwepo.”
Ingawa utafiti wao umeona hivyo bado wenyewe pia wanakubali ya kwamba kuna wanaoweza kupinga matokeo hayo. Na tayari wapo ambao wanasema bado njia pekee ya watu wanaovuta muda mrefu kufanikiwa kuacha ni kupitia matibabu yanayohusisha utumiaji wa dawa mbalimbali.
Utumiaji wa sigara za umeme, e-cigarettes, unakua sana duniani kote. Inasemekana Uingereza tuu kuna watumiaji takribani milioni 3.
Sehemu mbalimbali zinazotengeneza sigara za umeme
Tafiti nyingi zinaonesha sigara za umeme hazina madhara makubwa pale zikilinganishwa na sigara za kawaida. Shirika la Afya la Uingereza (Public Health England) linasema sigara za umeme ni asilimia 95 salama zaidi ukilinganisha na sigara za kawaida.
Je ushawahi kuziona au kutumia sigara hizi?
Sigara hizi zipo za aina mbalimbali kutoka makampuni mbalimbali
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon