Badilisha Akaunti Yako Ya Facebook Kuwa Page kwa Njia Rahisi zaidi

Swali: Ni Jinsi gani unaweza tengeneza
Facebook Page?
Tukiachana na hiyo je ushawahi sikia kuwa
unaweza badilisha akaunti yako ya facebook na
kuwa page? yaani watu wakaanza kuku ‘Like’
baadala ya kuku ‘Add As A Friend’. Najua
unaweza ukawa na maswali mawili hapo juu ya
kwanini na ni kwa vipi?.. Ngoja nikujibu Yote
Kama inavyojulikana Facebook ni moja kati ya
mitandao ya kijamii ambayo inatikisa dunia kwa
sasa. Licha ya hivyo pia Facebook wana
vipengele vingi sana na bado wanaendelea
kutoa vingine vingi ambavyo vinaifanya
Facebook izidi kuwa Juu.
Kwa Nini Ubadilishe Akaunti Yako Ya Facebook
Kuwa Page
Kama unatumia ukurasa wako wa facebook
kufanya biashara za mtu au hata kutangaza
biashara ya mtu si sahihi ni unakiuka vigezo na
masharti. Biashara zote inabidi zifanyike katika
‘Page’ na sio akaunti za kawaida kama
unazotumia. Kwa kifupi huruhusiwi kutumia
ukurasa wako wa facebook kuwasilisha kitu
kingine chochote kisichokuwa kinahusiana na
wewe kwa mfano biashara yako.
Kutokana na hayo basii unahitaji Page ili
utangaze na kuendesha biashara yako. Sasa si
vizuri kuanza na moja kabisa. Si unaweza tuu
kubadilisha akaunti yako ikawa ndio page yako.
Hii itakurahisishia kwa sababu hata watu
waliokuwa marafiki zako watakua ndio watu
wako wa kwanza kwanza kulike page hiyo
Pia kumbuka Facebook inaruhusu akaunti ya
kawaida kumiliki marafiki 5000 tuu lakini ukiwa
na page hata kufikisha bilioni inawezekana.
Sasa baada ya kujua sababu twende tukajua
tutafanikisha vipi jambo hili.
Jinsi Ya Kubadilisha Ukurasa Wako Wa
Facebook Kuwa Page
Kabla ya kuchukua maamuzi ya kuendelea ni
vyema kujua taarifa gani zitahama kutoka katika
ukurasa wako na kwenda samabamba katika
Page yako. — Hapa utajua nini kitabaki na nini
kitapotea —
Nini Kitahama
– Kama nilivyosema awali marafiki zako wote
na followers wako watakuwa ndio watu wanao ‘
like’ page yako
– Username Yako ndio itakuwa username ya
Page Yako
– Picha ya kwenye profile lako ndio itakua picha
ya kwenye Page yako
– Bado utakuwa na mamlaka sawa katika Page
zingine ambazo unaziendesha
Nini Hakitohama/Kitafutika
Post zako, Picha na Album zote hazitakuwa
zimehama bali zitafutika hivyo ITPhidel bloger
Nashauri uhifadhi taarifa zako zote kabla ya
kufanya zoezi hili
Pia utapoteza cheo chako katika makundi yote
ambayo yapo chini yako. Hivi tunashauri kuwa
kabla ya kufanya zoezi hili uchague mtu na
umeweke awe ndio mwendeshaji wa makundi
hayo.
Sasa unaweza kuendelea na kubadilisha akaunti
yako ya Facebook kuwa Page kwa kufuata
Maelekezo haya.
>Log in katika ukurasa wako wa facebook
>Fuata (bofya) Link Hii Kuanza kubadilisha
Akaunti yako kuwa Page
>Chagua Aina ya page unayotaka katika
machaguo yaliyojitokeza
>katika kuchagua aina ya page chagua pia
‘Category’ inayokufaa kisha bofya ‘Get
Started’
Safii sasa umefanikiwa
kubadilisha Akaunti yako ya
facebook kuwa page. Ni
matumaini yangu kuwa tatizo
lolote au ukikwama katika
kipengele chochote juu ya makala
hii utanishitua Rafiki yangu .

Previous
Next Post »

Ads Inside Post