Ongeza Ujazo Wa Uhifadhi (Memory) Katika Simu Yako Ya iPhone!

Mara kwa mara nimekuwa nikishauri kama wewe ni mtumiajia wa iPhone basi epuka kununua zile zenye GB 16 kwani hizo GB huwa hazitoshagi sana kwa simu janja kama hizi. Sawa nimekuwa nikisemaga hivyo lakini kuna wengine wanazo na wakifuata njia hii, wataifurahia
Njia hii kwa mara ya kwanza kabisa imegunduliwa na kuwekwa wazi katika mtandao wa Reddit. Wengi walioipokea nia hii kwa tabasamu kubwa ni wale ambao wana simu za GB 16, sawa hata kwa simu zenye ujazo mwingine njia hii inaweza ikafanya kazi
Naongea sana eeh? Haya ngoja tujionee jinsi tunavyoweza kupata ujazo wa uhifadhi wa ziada.
Nenda Katika Settings
Hapa itakubidi uenda katika ‘settings’ ili kujua umebakiwa na kiasi gani cha ujazo wa uhifadhi katika simu yako. Fanya hivi kwa kwenda kwenye Settings > General > About . Shuka chini mpaka kwenye Available ili kuona kiasi cha ujazo kilichosalia.
Kiasi Cha Ujazo Kilichobakia
Fanya Kama Unaazima Sinema (Movie)
Usishtuke, utakuwa huazimi sinema kama unavyofikia. Nenda katika sehemu ya iTunes Store na kisha tafuta sinema ambayo ina ujazo mkubwa kuliko ule uliouacha katika simu yako. Ukitaka kufanikiwa jambo hili kwa haraka itakubidi utafute (search) sinema ambazo zina matolea mengi kwa mfano sinema ya Lord Of The Rings.
Fanya Kama Unaazima Sinema
Pale utakapojaribu kuichukua siinema hiyo, utapa ujumbe ambao unasema kuwa huna ujazo wa kutosha ili kuichukua sinema hiyo. Ujumbe huo utakuwa umeambatana na machaguo mawili ambayo ni ‘OK’ na ‘Settings’
Nenda Tena Katika Settings
Kwa kubofya katika chaguo la ‘settings’ utaenda pale ambapo ulitoka mara ya kwanza. Cha kushangaza ni kwamba utaona muda huu kuna kiasi Fulani cha ujazo kimeongezeka ambacho ni tofauti na mwanzo wakati unaanza zoezi hili
Kinaweza kikawa kimeongezeka kwa kiasi kidogo sana lakini ukifanya njia hii mara kwa mara (mara nyingi) ujazo huo utaongezeka sana mpaka utafikia sehemu utakuwa hauongezeki tena.
Nini Hasa Kipo Nyuma Ya Pazia Kwa Jambo Hili?
Hapa ishu iliyopo ni kwamba ukifanya zoezi hilo simu yako (iPhone) inakuwa inafuta baadhi ya data kama vile zile za ‘Cache’ na zingine nyingi ili kutengeneza uwanja mkubwa wa ujazo wa kukuwezesha kulipia bidhaa husika (Sinema).
Kwa kutumia njia hii mpaka App zingine zinakuwa zinatumia kiasi kidogo katika kuhifadhi data. Kuna walioshuhudia App ya iTunes Store ikiwa inaandika ‘Cleaning’ (kwamba inajisafisha ili kupunguza data zisizokuwa na muhimu). Cha msingi ni kwamba simu inakuwa inasafisha taarifa ambazo sio za muhimu katika App tofauti tofauti katika simu.
Mpaka sasa nna imani utakuwa hutumii njia ya kufuta App zako unazozipenda ili kupata nafasi ya ziada kuweka App zingine unazozipenda zaidi. Kwa kutumia njia hii unaweza ukahifadhi vitu vyako vingi kama vile picha n.k. Kuna waliojaribu njia hii ikawaongezea mpaka GB 3.8 za uhifadhi

Previous
Next Post »

Ads Inside Post