Ongeza Kasi Ya Ushushaji (Download) Wa Vitu Kutoka uTorrent!

Vitu vingi kama vile vitabu, miziki, gemu mbaliimbali, sinema na kadhalika vinapatikana kwa uharhisi kupitia mitandao ya kukuwezesha kushusha mafaili ya torrent. Kwa kutumia programu kama vile uTorrent unaweza ukashusha mafaili hayo
Kuwa na uTorrent ni vizuri sana kwani utakuwa na uwezo wa kushusha mambo mengi sana ambayo unayahitaji. Lakini swala linakuja pale program hiyo inapokuwa na spidi ndogo katika kushusha mafaili hayo.
Muonekano Wa Ndani Wa uTorrent
Kutokana na kwamba mafaili hayo mengi yanasifiwa kuwa na ubora mzuri unaweza ukashangaa unapata tabu kuyasubiria ili yamalizike kujishusha. Kungojea huku kunakasirisha hasa kama unangoja sana kwa kitu ambacho unajua fika kingeweza kumaliza kujishusha masaa kadhaa yaliyopita.
Fanya Mambo Haya Ili Kuongeza Kasi Ya Ushushaji Katika uTorrent
1. Chagua ‘Port’ Yenye Spidi Kisha Ihifadhi
Ni jambo la muhimu sana kuchagua ‘port’ ambayo itakuwa inashusha mafaili mbalimbali ya torrent kwa haraka. Ukifanikiwa kuipata ‘port’ hiyo jambo jema hapo litakuwa ni kui ‘save’ (hifadhi) kwa matumizi ya baadae. Ili kufanya hivyo itakubidi uende katika uTotternt kisha chagua ‘Options’ na kisha ingia kwenye ‘Preferences’
Uchaguzi Wa ‘Port’
Chagua ‘Connection’ katik alist iliyotokea na window mpya itatokea. Chagua ‘Port’ moja lakini uwe na uhakika kuwa sehemu ya ‘Randomized Port Each Start’ iwe haijapigwa tiki. Ukifanya hivi itakusaidia katika kuongeza kasi ya ushushaji wa mafaili yako ya torrent kupitia uTorrent.
2. Zima FireWall
Hii ni moja kati ya njia rahisi kabisa za kuongeza kasi au spidi ya kushusha mafaili mbalimbali ya toreent kupitia uTorrent. FireWall kazi yake kuu ni kuzuia wadukuzi (hackers) na ‘software’ zinazoweza leta madhara katika kompyuta yako, kupata mwanya wa kuingia katika kompyuta yako kwa kutumia intaneti.
Jinsi Ya Kuzima ‘Firewall’
Ukifanikiwa kuizima bila shaka uTorrent itapata spidi zaidi katika kushusha mafaili ya torrents. Cha muhimu kukumbuka hapa ni kwamba ukishamaliza kushusha vitu vyako tuu, hakikisha unaiwasha tena ‘FireWall’ ili kompyuta yako iweze kuwa na ulinzi zaidi kama mara ya kwanza.
3. Tumia Toleo Jipya Kabisa La uTorrent
Kama unatumia toleo la zamani huna budi kusasisha au kama hujui kama unatumia toleo gani basi inakubidi utizame ile ujue kinachofuata. Ukiwa na toleo jipya kabisa unaweza ukapata kilicho bora zaidi kwani utakutana na maboresho mengi hii ikiwemo na kasi ya zaidi katika kushusha mafaili yako ya torrent
Sasisha uTorrent

Previous
Next Post »

Ads Inside Post